1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Utandawazi wasababisha mabadiliko makubwa katika maisha ya mwanadamu

Saumu Ramadhani Yusuf1 Machi 2010

Je ni zipi athari za Utandawazi

https://p.dw.com/p/MGFG
Makontena yamekuwa ni biashara kubwa kote duniani kutokana na utandawaziPicha: Alexander Klose

Madhara yanayosababishwa na Utandawazi yanadhihirika takriban katika pembe zote za maisha ya mwanadamu.Sio tu katika siasa na uchumi, bali hilo linajitokeza hata katika maisha ya kawaida ya kila siku. Hali hiyo inatoa ushahidi tosha kwamba kila mmoja anapasa kutafakari juu ya suala hilo.

Kinachodhihirisha kupanuka kwa utandawazi kutokana na ongezeko la matumizi ya bidhaa za viwandani ni Makontena makubwa ya usafiri ya upana wa mita sita au 12 na urefu wa mita 2.36. Biashara ya dunia inawezekana tu kupitia bidhaa ya chuma, bidhaa ambayo inaangaliwa kama ni nembo ya kuunganisha uhusiano wa mabara.Kwa mantiki hiyo, maonyesho ya Makontena pia yanaweza kuangaliwa kama aina fulani ya mwito wa sanaa katika utandawazi, kama anavyosema afisa wa usimamizi wa makumbusho ya Granska, Angeli Sachs.

''Kontena ni chombo ambacho ndani yake kina muundo wa wazi,ambao ukubwa wake unatumika kama mfumo wa usafiri ulioletwa na utandawazi. Kile kinachoonekana kama uwezekano wa kukaribia kuja kusahaulika kwa gharama za usafiri, kutokana na kwamba makampuni yenyewe yanaonekana kama ni miji ambayo inashirikiana katika utengenezaji, ukamilishaji, na usafirishaji. Na wakati huohuo, Kontena linaonekana kama linachukua nafasi ya kuwa chombo muhimu na mwafaka katika kuendelea kwa kazi hiyo''

Maduka mengi makubwa makubwa hii leo, kwa mfano, kama maduka ya IKEA yametengezwa kwa Makontena. Bidhaa za usafiri na za kufunga mizigo zinachukua nafasi kubwa katika biashara ya maduka hayo na bila shaka bidhaa hizo pia zinaharibu mazingira. Katika bahari ya Pasifiki kuna mzunguko wa takataka na hasa uchafu wa plastiki za kila aina zinazokusanywa kwenye eneo la Hawaii na baadae kusukumwa katikati ya bahari na kampuni kubwa ya kukusanya takataka ya Global Garbage Patch. Kampuni hiyo pia katika kipindi cha miaka 40 iliyopita imefanya mabadiliko makubwa kutoka kwenye enzi za kutumia meza za mbao na vifaa vya kuandikia pamoja na mashine za kupiga chapa na kuingia katika ulimwengu wa kisasa wa kutumia vifaa vingi vya umeme vinavyotoa huduma zote kwa wakati mmoja.Vifaa hivyo ni dhahidi kwamba ndio sura hali ya utandawazi-

Details des Containers
Kontena zimekuwa chombo muhimu cha usafiri katika ulimwengu wa biasharaPicha: DW

''Simu za mkononi, compyuta ndogo au Laptop, masanduku ya magurudumu. Viwanja vya ndege vya kisasa, Chupa za lita 0,5. Kuna vitu vingi ambavyo siwezi kumaliza kuvitaja ambavyo vinatumiwa na watu wanaosafiri ambavyo utengenezaji wake umebadilika''

Vifaa maalum vya kisasa kwa ajili ya usafiri vinamuhusu mfanya biashara na mtu anayesafiri sana. Anayekaa uwanja wa ndege akisubiri safari yake huku akiendelea na shughuli zake za kibiashara. Hata hivyo, pia kuna upande mbaya unaohusu mabadiliko hayo yanayoletwa na utandawazi kwa watu wanaosafiri kwa meli pamoja na wahamiaji ambao wako kama wasafiri waliofunikwa macho kuelekea katika ulimwengu wa kwanza kutafuta maisha. Sio tu maeneo yote ya kusubiri usafiri yako sawa kila mahala. Juu ya hilo, hata vipindi vya televisheni vimebadilika. Zamani kila taifa linatazama vipindi vya nchi yake lakini hilo limebadilishwa na utandawazi ambapo leo habari zinaweza kuonekana katika dunia nzima.

Kipindi, kwa mfano cha Big Brother, kinaigizwa katika nchi nyingi na hata vipindi vya muziki kama MTV vinatazamwa kote duniani. Hata hivyo, yote hayo yanasababisha ushindani mkubwa baina ya makampuni ya kikanda na kimataifa.

Mwandishi Gampert Christian ZR /Saumu Mwasimba

Mhariri: Othman, Miraji