1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa 20 wa kundi la dola la kiislamu wakamatwa

Amina Mjahid4 Agosti 2016

Mkuu wa Ujumbe wa wabunge wa Uturuki wanaoizuru Ubelgiji amesikitishwa na tukio la Umoja wa Ulaya kutoiunga mkono nchi hiyo kufuatia jaribio la kutaka kuipindua serikali katika nchi inayowania kujiunga na Umoja huo.

https://p.dw.com/p/1JbRd
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: Reuters

"Jaribio la kuipindua serikali limefanyika kwa mara ya kwanza katika nchi ambayo ipo kwenye majadiliano na Umoja wa Ulaya," alisema mkuu wa ujumbe huo Sena Nur Celik wa chama tawala cha AKP akiliita tukio hilo kama shambulio la demokrasia na thamani ya Ulaya.

Nur Celik amesema walitarajia wakuu wa nchi, Mawaziri na maafisa wa Umoja wa Ulaya kwenda Uturuki kujionea wenyewe kile kinachoendelea, kuliko kutegemea taarifa wanazoziona katika vyombo vya habari. "Sote tunajua mshikamano uliyoonekana wakati Ufaransa iliposhambuliwa, sidhani kama hatua kama hiyo ilionekana nchini Uturuki, tunasikitika sana," aliongeza Nur Celik.

Aidha amevikosoa baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti kuwa jaribio la mapinduzi ilikuwa njama iliyopangwa na serikali ili kudhibiti zaidi madaraka.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recep Tayyip ErdoganPicha: picture-alliance/AP Photo/Presidential Press Service/K. Ozer

Matamshi hayo yamejiri wakati wajumbe hao kutoka kamati ya masuala ya mambo ya nje ya bunge nchini Uturuki walipokutana mjini Brussels na wenzao wa Ubelgiji, maafisa wengine wa Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ubelgiji pamoja na mashirika yasio ya kiserikali. Juhudi za kuonana na maafisa wa Umoja wa Ulaya zilishindikana kwa sababu kipindi cha kiangazi tayari kimeshaanza mjini Brussels

Waziri John Kerry anatarajiwa kuizuru Uturuki mwishoni mwa Agosti

Huku hayo yakiarifiwa Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerrry anatarajiwa kuizuru Uturuki mwishoni mwa mwezi huu hii ikiwa ni kwa muhjibu wa shirika la habari la nchi hiyo CNN Turk, ziara hii inakuja zaidi ya mwezi mmoja baada ya jaribio la kuipindua serikali kuyatikisa mataifa wanachama wa NATO.

Uhusiano wa Uturuki na Marekani umeingia doa kufuatia jaribio hilo ambalo rais Tayyip Erdogan anadai lilipangwa na kiongozi wa kidini wa Uturuki aliyeuhamishoni nchini Marekani Fethullah Gulen. Rais Erdogan ameiomba Marekani kumrejesha Gullen nchini Uturuki. Hata hivyo Fethullah Gulen ameendelea kukanusha kuhusika katika jaribio lililofeli la kutaka kuipindua serikali.

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry
Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani John KerryPicha: Getty Images/AFP/J. Thys

Kwengineko Polisi ya Uturuki imetangaza kuwakamata washukiwa 20 wa kundi la wanamgambo wa dola la kiislamu kusini mwa mji wa Adana mapema hii leo. Kulingana na shirika la habari la Dogan nchini humo, polisi wa kupambana na ugaidi wakisaidiwa na helikopta walishambulia maeneo 22 ya kundi hilo baada ya kuarifiwa kuwa kundi hilo linapanga kufanya mashambulizi.

Kwa upande wake Rais Tayyip Erdogan amesema wanamgambo wa IS kutoka eneo lililokuwa Umoja wa Kisovieti walihusika katika shambulio lililotokea katika uwanja wa ndege wa Istanbul mwezi Juni lililosababisha watu 45 kuuwawa.

Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/dpa

Mhariri: Yusuf Saumu