1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yataka Palestina isaidiwe

Sudi Mnette
18 Mei 2018

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki ameitisha mkutano wa mataifa 57 wanachama wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu-OIC, kutokana na mauaji ya zaidi ya Wapalestina 60 yaliofanywa na majeshi ya Israel.

https://p.dw.com/p/2xxts
Türkei, Präsident Joko Widodo in OIC Istanbul
Picha: Laily Rachev/Biro Pers Setpres

Waandamanaji wa Kipalestina wanapinga kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem.Uturuki imeyataka mataifa ya Kiislamu yashikamane pamoja kuhusu Palestina na kushirikiana kuzizuwia nchi nyengine kujiunga na Marekani kuhamishia balozi zao zilioko Israel mjini Jerusalem kutoka Tel Aviv. Akihutubia mkutano huo wa mataifa ya Kiislamu, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amesema uamuzi wa Marekani ni haramu na umeipa nguvu Israel kuendelea kuwauwa Wapalestina wasio na hatia. Waziri huyo alisema pia kwamba panapaswa paweko na tahadhari katika Jumiya hiyo, baada ya baadhi ya mataifa kuunga mkono, kujizuwia au kutoonekana kabisa, wakati wa kupiga kura katika Umoja wa  Mataifa mwezi Desemba, juu ya uamuzi wa Marekani kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Wito wa Iran kwa nchi za OIC

Hassan Rouhani
Rais Hassan Rouhani wa IranPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Noroozi

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran, Javad Zarif alisema nchi za Kiislamu zinapaswa kushirikiana na mataifa mengine, kukabiliana na uhalifu wa Israel kwa Wapalestina na uamuzi wa Marekani kuuhamishia ubalozi wake Jerusalem.

Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizosimama kidete kuikosoa hatua ya Marekani pamoja na machafuko ya Gaza, huku serikali mjini Ankara ikitangaza maombolezi ya siku tatu kuwakumbuka waliouwawa. Rais Erdogan amevitaja vitendo  vya majeshi ya Israe kuwa ni" Mauaji ya Kimbari," na Israel kuwa "Dola la Kigaidi ". Matukio ya Gaza yamesababisha pia mgogoro wa kidiplomasia kati ya Uturuki na Israel, na  kila mmoja kumfukuza balozi wa upande mwengine. janga linalowakumba Wapalestina linawagusa wengi wa waturuki wakiwemo wenye msimamo wa Kizalendo na wa kidini miongoni mwa wapiga kura na ambao  ni ngome ya kisiasa ya erdogan, anayewania kuchaguliw atena katika uchaguzi wa rais mwezi ujao.

Wakati huo huo maelfu ya watu waliandamana mjini Istanbul leo kwa mkutano wa hadhara ulioitishwa na rais Erdogan, kuonyesha mshikamano na  Wapalestina na kulaani mauaji ya Israel Baadhi ya Viongozi na  mawaziri waliowasili kwa ajili ya mkutano wa kilele  wa Jumuiya ya nchi za kiislamu walishiriki kwenye maandamano hayo, akiwemo waziri mkuu wa Palestina Rami Hamdallah.

Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa  Zeid Raád al-hussein, amesema leo kwamba Israel kwa makusudi inawanyima Wapalestina haki  zao, huku milioni 1 na laki 9 walioko Gaza wakiishi sawa na kwenye p ango lenye sumu tangu kuzaliwa hadi kufa.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman/Reuters, Ap

Mhariri: Grace Patricia Kabogo