1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwekezaji wa aina mpya Afrika watajwa kuwa ukoloni mpya

21 Aprili 2009

Wawekezaji wawania ununuzi wa maeneo makubwa ya ardhi

https://p.dw.com/p/HbHA
Licha ya kuwa na eneo kubwa la ardhi ya kilimo nchini nyingi za Afrika hutegemea msaada wa chakula.Picha: AP

Nchi za Afrika kusini mwa jangwa la Sahara,hivi karibuni zimegeuka kuwa shabaha ya vitega uchumi vya aina mpya ambavyo ni masalio makubwa ya ukoloni. Wawekezaji kutoka nchi za viwanda na zile zenye uchumi unaoinukia kwa kasi, zinanunua au kukodisha maeneo makubwa ya ardhi kote barani humo, ama kuhakikisha mahitaji yao wenyewe ya chakula au kwa ajili ya biashara nyengine.

Katika kufikia lengo lao hilo la kujipatia maeneo makubwa ya ardhi, wawekezaji hao hushirikiana hata na vigogo ambao hudai kuwa na mamlaka ya mali hizo, kama ilivyo nchini Sudan kwa mfano.

mashirika yasiokua ya kiserikali na wanaharakati barani ulaya wanalaani mtindo huu wa kutwaa ardhi nchini Misri, Sudan, Cameroun, Senegal, Msumbiji na kwengineko barani Afrika, wakisema ni aina mpya ya ukoloni.

Mtafiti wa kijerumani Uwe Hoering anayehusika na sera ya maendeleo kwa ajili ya mashirika kadhaa yasiokua ya kiserikali barani Ulaya pamoja na kijijarida kipya Weltwirschaft un Enwitcklung-Uchumi wa dunia na maendeleo- ameviita vitega uchumi hivyo vibaya kuwa ni aina mpya ya kile alichokiita "ukoloni wa kilimo."

Katika mahojiano na shirika la habari IPS, Bw Hoering alisema mtindo wa kutwaa maeneo ya kilimo barani Afrika, ulianza kuonekana wazi 2008 kama matukio ya kile kinachoonekana kuwa ni mbio za utengenezaji wa mafuta kutokana na mimea na mfuko wa bei na uhaba wa chakula.

Ingawa wawekezaji wanazilenga pia ardhi zenye rutuba katika maeneo mengine duniani, hata hivyo eneo la Afrika kusini mwa janga la Sahara linaelekea kuwa shabaha kuu ya wawekezaji hao. Sababu ni nyingi:-

Kwa upande mwengine Afrika ina akiba kubwa ya ardhi anasema Bw Hoering. Kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa, ni asili mia 14 tu ya ardhi bora ambayo inatumika kwa kilimo wakati huu.Zaidi ya hayo anasema serikali nyingi barani Afrika ziko tayari kuruhusu ardhi zao zitwaliwe na wawekezaji hao.

Bazaruto and Benguerra Island - Mozambique
Kisiwa cha Bazaruto and Benguerra Island Msumbiji ni kivutio kimoja wapo cha wawekezajiPicha: Cynthia Cavalcanti

Kwa mujibu wa orodha katika ripoti ya mwaka jana 2008 ya Shirika la lisilokua la kiserikali la GRAIN lenye makao yake makuu mjini Barcelona-Uhispania, ni kwamba nchi ambazo uchumi wao unakua haraka kama China na India na pia nchi zinazotoa mafuta kwa wingi kwa mfano za kiarabu katika Ghuba na hata Libya, zinanunua maeneo makubwa ya ardhi barani Afrika.

Lengo la nchi hizo ni kuhakikisha usalama wao wa chakula ,kwani Bw Hoering anasema baada ya utabiri hivi karibuni kuhusu hali ya nafaka na chakula katika masoko na kupanda mno kwa bei, nchi hizi zimepoteza imani katika soko la dunia. sasa zinataka kuwa na uwezo wa kudhibiti na kuhakikisha usalama wa chakula zinazoagiza. Aidha sambamba na hayo, kupanda kwa bei ya chakula duniani kumeimarisha kasi ya wawekezaji hao wa kigeni, kuwania udhibiti wa maeneo zaidi ya ardhi zenye rutuba barani Afrika.

Mwezi Septemba mwaka jana taasisi ya fedha ya kimataifa International Finance Cooperation -IFC- tawi la uwekezaji wa biashara la benki ya dunia ilitangaza kwamba itaongeza mno uwekezaji katika maendeleo ya biashara ya kilimo barani Afrika na katika mataifa ya Amerika kusini na Urusi, kwa sababu ya nia ya sekta mpya ya binafsi ya kutaka kufaidika zaidi kutokana na mgogoro wa chakula.

Kwa upande wake Shirika hilo la GRAIN ambalo ni la kimataifa pia limesema kuna makampuni makubwa ya binafsi ya kimataifa yanayohusika katika biashara hiyo, kama Blackstone, Deutsche Bank, na Goldman na Sachs ambayo yanashiriki katika mpango wa kutenga maeneo makubwa ya kilimo hicho kipya ndani barani Afrika.

Chini ya zingatioo ya hali hiyo,wakosoaji wanasema,"huu ni ukoloni wa aina mpya."

Mwandishi:Mohammed Abdul-Rahman/IPS

Mhariri:Josephat Charo