1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vazi alilovalishwa Obama ni la kitamaduni sio la kidini

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DL9S

NAIROBI

Mzee wa Kenya ambaye alimzawadia Seneta Barack Obama wa Marekani vazi la jadi amesisitiza kwamba vazi hilo lilikuwa la kitamaduni na sio la kidini.

Picha za Obama akiwa amevaa kanzu na kilemba zilisambazwa kwa wingi kwenye mtandao na mwandishi wa kisiasa kwenye mtandao nchini Marekani amesema amezipata picha hizo kutoka waajiri wawili wasiotajwa majina wa mpinzani wa Obama katika kuwania tiketi ya kuwania Urais wa Marekani Hilary Clinton.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo wamedokeza kwamba picha hizo zilimuonyesha Obama kuwa ni Muislamu lakini mtumishi mstaafu wa serikali Mohammed Hassan Mumin amesema katika makala iliochapishwa leo hii na gazeti la The Nation la Kenya kwamba aliwahi kuwapa zawadi za nguo kama hizo viongozi wengine kadhaa wakiwemo marais watatu wa Kenya na mtu mmoja wa familia ya kifalme ya Uingereza.

Amesema ingelikuwa Rais Bush atakwenda Kenya angelimvalisha vazi kama hilo alilomvesha Obama.