1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vibonzo vya kumkosoa rais nchini Rwanda ni marufuku

Bruce Amani
25 Aprili 2019

Mahakama kuu nchini Rwanda imetupilia mbali madai yalikokuwa yametolewa na baadhi ya wanasheria nchini humo kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/3HQRX
190213 Infografik Cartoon Kagame Hands over AU Chair to Sisi

Mahakama kuu nchini Rwanda imetupilia mbali madai yalikokuwa yametolewa na baadhi ya wanasheria nchini humo kupinga sheria iliyoanzishwa mwaka jana kuwa ni kosa la jinai kuchora vibonzo vinavyomkejeli Rais wa nchi hiyo. Wakati huohuo wanasheria wamefungua kesi kulipinga hilo huku wakisema masharti hayo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo. Kuanzishwa kwa sheria hiyo pia kulizusha malalamiko mengi kutoka kwa waandishi wa habari wakisema sheria hiyo inahatarisha uhuru wao wa kufanya kazi. Sasa mahakama kuu imetoa hukumu ambayo inasema kuchora kibonzo kinachomkejeli Rais kwa njia yoyote ile litaendelea kuwa kosa la jinai.

Soma zaidi ...

Hata hivyo mahakama hiyo imeamua kuwa viongozi wengine waandamizi serikalini na pia viongozi wakuu wa kidini halitakuwa kosa la jinai kuwachora kwenye vibonzo. Mkuu wa jopo la mawakili waliokuwa wameishitaki serikali kuhusu sheria hiyo Richard Mugisha amesema wao kama wanasheria wameridhika na uamuzi wa kuondolewa baadhi ya vipengele kwenye sheria hiyo.