1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Baba mtakatifu anazuru Austria

7 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBS3

Baba mtakatifu Benedict wa 16 yuko mjini Vienna kwa ziara ya siku tatu nchini Austria.

Leo ametembelea mnara wa wahanga wa mauaji ya kifashisti.

Baba mtakatifu amekutana na rais Heinz Fischer wa Austria na kansela Alfred Gusenbauer na viongozi wengine mashuhuri.

Ziara yake inajumuisha pia ibada kubwa ya hapo kesho siku ya jumamosi katika eneo takatifu la Mariazel.

Eneo hilo lilianzishwa miaka 850 iliyopita na linahudhuriwa na mahujaji wengi kila mwaka.