1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vienna. Iran imepiga hatua kuelekea uwazi kwa mradi wake wa kinuklia; Ripoti.

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CI1e

Ripoti iliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa la nishati ya Atomic imesema kuwa Iran imepiga hatua muhimu kuelekea uwazi juu ya mpango wake wa kinuklia. Lakini shirika hilo la umoja wa mataifa pia limeonya kuwa nchi hiyo bado haijatatua masuala muhimu ambayo hayajafafanuliwa.

Ripoti hiyo , ambayo imetolewa kwa bodi ya shirika hilo yenye wajumbe 35, imesema kuwa Iran inaendelea na kulipinga baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kupuuzia madai yake muhimu ya kusitisha shughuli zake za urutubishaji wa madini ya uranium.Marekani na umoja wa Ulaya zimetishia kuiwekea vikwazo vipya Iran , hadi pale itakapojisafisha kuhusu mpango wake huo wa kinuklia. Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Zalmay Khalilzad ameionya hata hivyo China dhidi ya upinzani wake kwa vikwazo vya umoja wa mataifa kwa Iran.

Siamini kuwa China itataka kuwa kikwazo katika njia ya diplomasia ya kweli kupambana na suala hili, kwasababu ni azimio imara tu likiambatana na vikwazo vikali , litatoa nafasi kwa diplomasia kupata mafanikio.