1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA: Waziri wa mambo ya ndani wa Austria afariki mkesha wa mwaka mpya.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe7
Jiji la Dar es Salaam palipofanyika Semina ya ukaguzi wa fedha
Jiji la Dar es Salaam palipofanyika Semina ya ukaguzi wa fedhaPicha: DW /Maya Dreyer

Waziri wa mambo ya ndani wa Austria, Liese Prokop, amefariki mkesha wa mwaka mpya alipokuwa akipelekwa hopitalini baada ya mshipa wa moyo wake kupasuka.

Duru zinasema waziri huyo mwenye umri wa miaka sitini na mitano alikuwa akishiriki kwenye mazungumzo ya kuundwa serikali mpya kutokana na uchaguzi uliofanywa Oktoba mosi.

Waziri huyo ni mwanachama wa chama cha People’s Party cha kansela anayeondoka madarakani Wolfgang Schuessel.