1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifaru vya Israel vimeingia Ukanda wa Gaza

12 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CaSC

GAZA:

Wanamgambo 5 wa Kipalestina wameuawa kwenye Ukanda wa Gaza baada ya Israel kuzindua operesheni kubwa ya kijeshi katika eneo la kusini linalodhibitiwa na Hamas.Mashambulizi hayo yamefanywa siku moja kabla ya wapatanishi wa Israel na Palestina,kukutana kwa mara ya kwanza tangu majadiliano ya amani kuanzishwa rasmi mwezi uliopita nchini Marekani.

Kwa mujibu wa mashahidi na duru za hospitali, wanachama 3 wa kundi la Islamic Jihad waliuawa baada ya kushambuliwa na kifaru cha jeshi la Israel,huku kama vifaru 30 vikijipenyeza ndani ya Ukanda wa Gaza.Muda mfupi baadae katika eneo hilo hilo,wanamgambo wengine 7 walijeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Israel.