1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vigogo wa CCM wahamia CHADEMA

13 Oktoba 2010

Wakati CCM ikizindua kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, kuna taarifa za baadhi ya vigogo wake kukihama chama hicho tawala na kukimbilia kwenye vyama vya upinzani, hasa CHADEMA.

https://p.dw.com/p/PCYR

Mwishoni mwa wiki chama tawala cha CCM kilizindua rasmi kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010. Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nacho kinatazamiwa kuzindua rasmi kampeni zake mwishoni wa juma hili mjini Dar es Salaam. Lakini, tayari chama hiki kimevuna baadhi ya vigogo wa CCM ambao wamekiacha mkono.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam George Njogopa alibahatika kukutana na mgombea wa urais wa chama cha CHADEMA Dr Wilbrod Slaa aliyekuwa na mengi ya kuelezea.