1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vigogo wa Kenya waelekea ICC,The Hague

5 Aprili 2011

Washukiwa wa ghasia baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007 nchini Kenya waelekea The Hague, Uholanzi.

https://p.dw.com/p/10npH
ARCHIV - Das Gebäude des Internationalen Strafgerichtshofs (IStGH) in Den Haag (Archivfoto vom 29.03.2004). Der IStGH will am Mittwoch (04.03.2009) bekanntgeben, ob er gegen den sudanesischen Präsidenten Al-Baschir Haftbefehl wegen des Verdachts auf Kriegsverbrechen und Völkermord in der sudanesischen Krisenprovinz Darfur erlässt. Foto: Toussaint Kluiters (zu dpa 0282 vom 03.03.2009) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Jengo la ICC mjini The Hague, UholanziPicha: dpa

Hatma ya washukiwa sita wanaotuhumiwa kupanga na kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya, waliotajwa na mwendesha mashtaka wa mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Louis Moreno Ocampo wanaanza safari yao leo kuelekea mjini The Hague, Uholanzi wanakotarajiwa kwenda kujibu mashtaka hayo. Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta na Mbunge wa Eldoret Kaskazini, William Rutto wanaondoka leo usiku kuelekea The Hague. Hisia mbalimbali zimetolewa na viongozi pamoja na wananchi kuhusiana na kufikishwa mahakamani kwa washukiwa hao.

Mwandishi wetu Alfred Kiti Kutoka Nairobi ametuandalia taarifa hiyo.

Mwandishi: Alfred Kiti

Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri:Abdul-Rahman