1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana na suruali mlegezo

11 Septemba 2012

Mtindo wa uvaaji wa suruali katikati ya makalio unazidi kuwa maarufu miongoni mwa vijana wengi wa kiafrika licha ya kukosolewa na jamii na hata kupigwa vita huko ulikoanzia, Kulikoooni!!

https://p.dw.com/p/166gG
group of graduation students in the park looking happy graduation; group; students; friends; women; men; diploma; academic; achievement; adult; attractive; beautiful; beauty; cap; certificate; cheerful; college; completion; cute; degree; education; female; girl; gown; diversity; group; graduation; graduate; happiness; happy; high; highschool; joy; joyful; people; portrait; pretty; ribbon; robe; school; scroll; smile; smiling; success; university; white; woman; young; youth; goal; congratulations; latin; american; hat; mortar; board; bachelors; student; man; graduates; women; men
Symbolbild Absolventen USA Studenten SchülerPicha: Fotolila/Andres Rodriguez

Katika Afrika Mashariki mtindo huu hujulikana zaidi kama mlegezo au kata K na ni miongoni mwa baadhi ya vijana wanaopenda kuvaa nguo za ndani maarufu kama Boxer. Kwa mujibu wa Greg Mathis, mtindo wa mlegezo uliigwa kutoka mfumo wa magereza nchini Marekani ambako mikanda ilipigwa marufuku katika magereza ili kuzuia wafungwa kujinyonga. Lakini mtindo huu ulikuja kupewa umaarufu na wasanii wa muziki wa hip-hop katika miaka 1990 na tangu wakati huo umekuwa kama alama ya uhuru na utambuzi wa kitamaduni, au alama ya kukataa maadili ya jamii kubwa.

Mathis pia anaupa tafsiri ya ngono mtindo huu katika magereza, akisema wale wanaoshusha suruali zao zaidi na kuonyesha makalio yao wanahamasisha wengine. Lakini kwa mujibu wa mtandao wa Snopes.com, hizo ni hadithi za mjini tu. Wakati wa muongo wa kwanza wa karne ya 21, serikali nyingi za mitaa, shule na hata mashirika ya ndege nchini Marekani yalipitisha sheria zinazopiga marufuku uvaaji wa suruali za mlegezo. Hata serikali za majimbo na serikali ya shirikisho ilipiga marufuku jambo hilo.

Heshima ya suruali ni pale inapofikakiunoni.
Heshima ya suruali ni pale inapofikakiunoni.Picha: picture-alliance / united-archiv

Rais Barack Obama, akizungumza na kituo cha MTV kabla ya uchaguzi wa mwaka 2008, alisema sheria zinazopiga marufuku uvaaji wa suruali za mlegezo zilikuwa sawa na kupoteza muda, lakini alifuatisha matamshi hayo na: "Baada ya kusema hayo, kina kaka laazima wapandishe suruali zao. Unatembea sambamba na mama yako, na bibi yako, chupi yako inaonekana, tatizo ni nini? Baadhi ya watu hawapendi kuona chupi yako, na mimi ni mmoja wao."

Mwezi Juni mwaka 2007 mji wa Delcambre, Louisiana ulipitisha sheria ya ufichuaji usiyo wa heshima, ambayo ilipiga marufuku uvaaji wa suruali wenye maksudio ya kuonyesha chupi. Machi mwaka 2008 halmashauri ya jiji la Hahira katika jimbo la Georgia ilipitisha sheria ya mavaazi yenye utata ambayo inapiga marufuku raia kuvalia suruali chini ya kiuno na kuonyesha ngozi au nguo za ndani. Kura za madiwani zilifungana na sheria ikapita kwa kura ya meya wa jiji hilo.

Watetezi wa suruali mlegezo
Lakini watetezi wa haki za binaadau walisema sheria hizi zilikuwa zinawalenga watu weusi na kuelezea hofu ya kuhusisha uvaaji wa mtu na makosa yanayotendeka. Wakosoaji wa uvaaji huu wa suruali wanauchukulia kama ulimbukeni wa vijana wa Afrika mashariki kuiga kila wanachokiona kutoka kwa wazungu. Saidi Mwishe ni kijana kutoka Dar es Salaam na hapa anatoa maoni yake kuhusiana na uvaaji wa suruali mlegezo.

Kulegeza suruali ni ukiukaji wa mfumo wa uvaaji katika baadhi ya shule na upigaji wake marufuku umeungwa mkono na mahakama nchini Marekani. Wiki mbili tu baada ya kutolewa kwa video ya kibao cha Pants on the Ground, bango la kampeni ya uhamasishaji dhidi ya mtindo wa kulegeza suruali lilwekwa katika jiji la Dallas, jimboni Texas. Bango hilo linamuonyesha mshiriki wa filamu ya Soul Food ya mwaka 1997, Big Mama Joseph akisema zivuteni juu na kuwaomba vijana wadogo kulitunza jambo hili kama siri. Kampeni hii ilibuniwa na Meya wa jiji la Dallas na inatumia nafasi ya matangazo iliyodhaminiwa na kamouni ya Clear Channel.

Bango lingine linalohamasisha dhidi ya kulegeza suruali lilizinduliwa mjini Brooklyn na seneta wa jimbo la New York Eric Adams Machi 28 mwaka 2010. na mei mwaka huo, rais wa seneti ya New York Malcolm Smith alitumia dola 2,200 kutoka mfuko wake wa kampeni kuzindua kampeni kama hiyo mjini Queens. Twaibu kalungi ni mwalimu somo la Kiingereza katika shule za DYCCC jijini Dar es Salaam, na anakiri kuwa tatizo la uvaaji huu wa suruali limekuwa kubwa miongoni mwa wanafunzi wa shule. Hii imewalaazimu kuchukua hatua kukomesha tabia hii.

Mteja akitizama suruali kwa nia kununua.
Mteja akitizama suruali kwa nia kununua.Picha: AP Photo

Hatua zaidi dhidi ya suruali mlegezo
Katika mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2010 mjini Vancouver, mshiriki wa mchezo wa skii kutoka Japan Kazuhiro Kokubo alizuiwa kushiriki katika sherehe za ufunguzi kutoka na kuvaa nguo za mtelezo ikiwa ni pamoja na suruali ya mlegezo. Mwishoni mwa mwaka wa 2010 shule ya kati ya Westside mjini Memphis, Tennessee, ilianzisha kampeni ambapo walimu wanvuta suruali zao juu na kuzishikiza huko, ambapo wanafunzi huchukua picha za walimu hao na kuzibandika katika mbao za madarasi ili wenzao wone. Katika mahojiano na kituo cha Televisheni cha WMC-TV, mkuu wa shule hiyo Bobby White alisema lengo la kampeni hiyo ni kupambana na utamaduni wa kisasa kwa kutumia njia zinazofanana na utamaduni huo.

Novemba 23 mwaka 2010, jiji la Opa-Locka, Florida, lilikubaliana kwa pamoja juu ya faini ya dola 250 au saa za kumi za kufanya kazi za kijamii kwa watu wasiyovuta suruali zao juu. Na mjini Fort Worth, Texas, mamlaka ya usafiri iliweka sheria inayowazuiya abiria wenye suruali za mlegezo zinazoonyesha chupi au makalio yao kupanda katika mabasi. Matangazo yalibandikwa katika mabasi hayo yakisema zivuteni juu au tafuteni usafiri mwingine. Msemaji wa mamlaka hiyo alisema siku ya kwanza ya kutekeleza sheria hiyo, watu 50 walishushwa katika mabasi kwa uvaaji usiyofaa. Lakini nani alaumiwe hasa kwa uvaaji huu usiyoendana na maadili ya kiafrika.

Katika jimbola Florida, sheria mpya ya jimbo ilianza kutekelezwa kwa mwaka wa masomo wa 2011-2012 ikipiga marufuku vitendo vya kulegeza suruali shuleni. Wanfunzi wanaokutwa wakilegeza, hupewa onyo ya mdomo kwanza, kisha wazazi wao hutaarifiwa kimaandishi na mkuu wa shule kwa kosa la pili ambapo mzazi atatakiwa apeleke nguo za kubadilishia shuleni. Kwa kosa la tatu, mwanafunzi anasimamishwa masomo kwa muda.

Mwanamitindo Naomi Campbell wa Uingereza.
Mwanamitindo Naomi Campbell wa Uingereza.Picha: AP

Kampuni za ndege nazo zawakataa wenye melgezo
Kampuni nyingi za ndege nchini Marekani pia zimewashusha abiria kadhaa kwa uvaaji wa suruali mlegezo kupilitiza. Mwezi Juni mwaka 2011, mchezaji wa mpira wa chuo kikuu cha New Mexico Deshon Marman alishushwa kutoka katika ndege ya shirika la ndege la Marekani kwa kuvaa suruali mlegezo. Hii ilifuatiwa na mwanamuzi Billio Joe Armstrong alieondolewa katika ndege ya shirika la South West kutoka Oakland kwenda Burbank California kwa kuvaa suruali mlegezo.

Na Aprili mwaka huu, jaji mjni Alabama alimhukumu kijana mwenye umri wa miaka 20, LaMarcus Ramsey, kwenda jela kwa siku tatu kwa kuingia mahakamani akiwa amevaa suruali ya mlegezo inayoonyesah chupi yake akimuambia umeidharau mahakama kwa vile umeonyesha makalio yako mahakamani. Na nchini Tanzania, kijana Rajabu Athumani mwenye umri wa miaka 20 alihukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio.

Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi ya ubakaji iliyokuwa inamkabili, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana. Msanii Suma G pamoja na ukweli yeye wakati mwingine huvaa suruali au kaptura mlegezo, haoni kama jambo linalostahili kufanywa na vijana wa kiafrika.

Aina mbalimbali za suruali zikiwa katika makumbusho ya mavazi ya Levi.
Aina mbalimbali za suruali zikiwa katika makumbusho ya mavazi ya Levi.Picha: AP

Wanamuziki wa Marekani pia wamedhihaki uvaaji wa suruali za mlegezo. Mwaka 1996 wimbo wa Back pockets on the Floor uliyopigwa na kundi la green Borthers liliponda uvaaji wa mlegezo na mwaka 2007 wimbo wa Dewayne Brown wa Pull your pants up ulikuwa na ujumbe sawa na huo. Januari mwaka 2010 Jenerali Larry Platt alipiga wimbo wa Pants on the Ground wakati wa majaribio ya sauti kwa ajili ya shindano la American idol mjini Atlanta, Georgia.

Ni jukumu lako wewe kama kijana wa kiafrika kupima jambo unalotaka kufanya ili kuona kama lina manufaa yoyote kwako binafsi na hata kimaadili, ukijua kuwa wewe ni kiongozi anayefuata wa taifa lako. Yale unayofanya ukiwa kijana, yatakuja kuwa na athari kwa maisha yako ya baadae.

Mwandishi: Iddi Sessanga
Mhariri: Josephat Charo