1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wafanya kampeni ya amani Lamu

Josephat Nyiro Charo1 Agosti 2014

Kampeni hiyo ilianzishwa kufuatia mauaji ya kutisha huko Mpeketoni, Hindi na Gamba katika kaunti ya Lamu, mwezi Juni mwaka huu wa 2014 ambapo watu zaidi ya 90 walipoteza maisha.

https://p.dw.com/p/1CnN8
Mpeketoni Kenia Anschlag Massaker
Picha: Reuters

Mtandao wa Vijana katika kaunti ya Lamu huko pwani ya Kenya, Lamu County Bunge Network, umeanzisha kampeni ya kushajiisha wananchi wa jimbo hilo kuhusu amani. Kampeni hiyo iliyopewa jina - "We are One - yaani Sote Ni Wamoja" - ilianza rasmi Julai 21 mwaka huu na tayari imefanyika katika miji ya Mpeketoni, Witu, Mokowe na Shela katika kisiwa cha Lamu. Vijana wa mtandao huo wamekuwa wakihubiri amani kupitia maonyesho ya mabarabarani na mikutano ya hadhara katika miji mbalimbali wakitumia tingatinga moja walilopewa na serikali ya kaunti ya Lamu, kwa kuwa baadhi ya maeneo hayafikiki kwa kutumia magari kutokana na hali mbaya ya barabara. Josephat Charo amezungumza na Mwenyekiti wa Mtandao huo wa vijana, Michael Kanja, ambaye kwanza anaelezea kuhusu kampeni hiyo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Khelef