1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Ethiopia vyatuhumiwa kufanya uhalifu wa kingono

Saleh Mwanamilongo
12 Agosti 2021

Makumi ya wanawake wanaelezea unyanyasaji wa kutisha uliofanywa katika mzozo wa jimbo la Tigray, inaelezea ripoti mpya ya shirika la Amnesty International.

https://p.dw.com/p/3yv6Q
Jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia limekuwa likikumbwa na ghasia tangu Novemba
Jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia limekuwa likikumbwa na ghasia tangu NovembaPicha: Nariman El-Mofty/AP/picture alliance

Zaidi ya visa 1,200 vya unyanyasaji viliripotiwa na vituo vya afya jimboni Tigray mnamo Februari na April pekee,linaelezea shirika la Amnesty International. Hakuna anayefahamu idadi kamaili ya watu waliofanyiwa dhulma hizo mnamo kipindi cha miezi tisa ya machafuko kwenye mkoa huo wa wakaazi milioni sita ambako vituo vya afya viliporwa na kuharibiwa.

Shirika hilo la haki za binadamu limesema idadi hiyo labda ni sehemu ndogo tu ya ukweli.Amnestyiliwahoji wanawake 63,pamoja na wanfayikazi wa afya. Wanawake kadhaa walielezea kushikiliwa kwa siku au wiki kadhaa huku wakibakwa na waume wengi mara nyingi. Wanawake wingine 12 walisema walibakawa mbele ya wanafamilia.

Wanawake wengine watano walisema walikuwa wajawazito wakati walipovamiwa. Na wawili walihadithia kwamba walikuwa na changarawe na risasi zilizoingizwa ndani ya sehemu zao za siri.

"Sijui ikiwa waligundua nilikuwa mtu," mwanamke mmoja aliliambia shirika la Amnesty. Akielezea jinsi alivyoshambuliwa nyumbani kwake na wanaume watatu. Wakati huo alikuwa na mimba ya miezi minne.

Uhalifu wa kingono silaha za vita ?

Wahanga wengine walisema walifanyiwa vitendo hivyo vya kinyama mbele ya familia zao
Wahanga wengine walisema walifanyiwa vitendo hivyo vya kinyama mbele ya familia zaoPicha: YASUYOSHI CHIBA/AFP

 Fisseha Tekle, Mtafiti wa shirika la Amnesty kwenye Pembe ya Afrika amesema visa hivyo vilifanywa na watu ambao walitakiwa kuwakinga raia.

''Askari walikuwa wakiwadhulumu waathirika, walikuwa wakiwapiga, walikuwa wakitumia udhalilishaji maneno au matusi ya kikabila dhidi ya waathiriwa ambayo yanaonyesha kuwa unyanyasaji wa kijinsia ulitumiwa kutowathamini wanawake wa Tigray katika mzozo unaoendelea. ", alisema Tekle.

Shirika la habari la Associated Press, limesema lilizungumza kando na wanawake ambao walielezea

kubakwa na genge na wapiganaji wanaoshirikiana na jeshi laEthiopia, haswa wanajeshi kutoka nchi jirani ya Eritrea lakini pia wapiganaji wa mkoa wa Amhara.

Shirika la haki za binadamu la Amnesty International limesema bado halijapokea tuhuma dhidi ya vikosi vya Tigray, ambavyo vilipata tena udhibiti wa eneo kubwa la Tigray mwishoni mwa Juni.

Amnesty inataka uwajibikaji kufuatia visa hivyo vya unyanyasaji wa jinsia. Imeomba pia visa hivyo kuorodheshwa kama uhalifu wa kivita. Katika taarifa baada ya ripoti hiyo, serikali ya Ethiopia ilisema hapo awali kwamba baadhi ya wanajeshi wake walihusika katika mienendo ambayo ni kinyume na sheria na maelekezo waliyopewa.