1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikwazo vipya dhidi ya Iran

P.Martin26 Oktoba 2007

Marekani imeweka vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Iran,ikiilaumu kuwa inajaribu kutengeneza silaha za kinyuklia na inaunga mkono ugaidi katika nchi za ngámbo.

https://p.dw.com/p/C77U
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice alipotangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran akiwa pamoja na Waziri wa Fedha,Henry Paulson
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Condoleezza Rice alipotangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran akiwa pamoja na Waziri wa Fedha,Henry PaulsonPicha: AP

Vikwazo vilivyotangazwa na Waziri wa Nje wa Marekani,Condoleezza Rice na Waziri wa Fedha Henry Paulson mjini Washington,vinalenga benki tatu za Iran,makampuni tisa yanayohusika na petroli,ujenzi na usafiri yanayodhibitiwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi-IRGC.

Condoleezza Rice amesema,vikwazo hivyo humaanisha hakuna raia au shirika binafsi la Kimarekani litakaloruhusiwa kuwa na shughuli za kibiashara pamoja na hao waliotajwa.Na mali yao iliyo chini ya mamlaka ya Marekani,itazuiliwa moja kwa moja.

Kwa upande mwingine,Rais wa Urusi,Vladimir Putin amesema,vikwazo vipya vya kimataifa dhidi ya Iran vitazidi kuchafua hali ya sasa.Iran,mara kwa mara imesisitiza kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu.