1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Cyprus mbili washindwa kuafikiana

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E53K

NICOSIA

Viongozi wa visiwa viwili vya Cyprus vilivyogawika wameshindwa kukubaliana juu ya tarehe ya kuanza mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu suala la kukiunganisha tena kisiwa hicho cha Mediterranean.Rais wa Ugiriki Dimitris Christofias na mwenzake wa Cyprus ya Uturuki Mehmet AlI Talat wametoa tangazo hilo kufuatia mkutano mjini Nicosia.Mazungumzo rasmi ya mwanzo yalitazamiwa huenda yakaanza mwezi ujao lakini katika wiki za hivi karibuni Christofias amekuwa akielezea kuvunjwa moyo kwake juu ya kushindwa kufanikiwa mazungumzo ya maandalizi ambayo yalikuwa yanawahusisha makundi kutoka Cyprus zote mbili.Kisiwa hicho kimegawika vipande viwili tangu mwaka 1974 baada ya Uturuki kuvamia eneo la kaskazini la kisiwa hicho kwa lengo la kujibu mapinduzi yaliyoongozwa na Ugiriki yaliyokuwa na azma ya kukiunganisha kisiwa hicho na Ugiriki.