1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Israel na Palestina wakubali mazungumzo

6 Machi 2008

-

https://p.dw.com/p/DJFw

GAZA

Mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na yale ya maendeleo yamefahamisha kwamba hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imezorota zaidi tangu mwaka 1967 wakati Israel ilipokalia ardhi ya eneo hilo.Mashirika hayo yakiwemo Amnesty International,na Save The Chldren yameikosoa hatua ya Israel ya kuweka vizuizi dhidi ya Gaza wakiikitaja kitendo hicho kuwa haramu ambacho kinawaathiri wasiokuwa na hatia.Israel lakini inatetea hatua yake ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza ikisema ni halali na inahitajika kwa ajili ya kuzuia mashambulio ya roketi ya wanamgambo wakipalestina.

Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolleza Rice aliyekamilisha ziara yake mashariki ya kati alifanikiwa hapo jana kuwashawishi viongozi wa Israel na Palestina kurudi kwenye meza ya mazungumzo ambayo yalikwamishwa na hali hiyo katika Gaza.Rais Mahmoud Abbas wa Palestina alisimamisha mazungumzo hayo na serikali ya Israel mwishoni mwa wiki baada ya Israel kuanzisha opresheni ya kijeshi ukanda wa Gaza ambayo ilisababisha kuuwawa kwa zaidi ya wapalestina 120.