1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa kidini wasaka amani Tana River

15 Januari 2013

Viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kutoka Mkoa wa Pwani nchini Kenya wanatarajia kufanya ziara katika eneo la Tana River katika jitihada za kutafuta amani kwenye eneo hilo lenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

https://p.dw.com/p/17K7j
Mkaazi wa Tana River akionesha magamba ya risasi walizoshambuliwa.
Mkaazi wa Tana River akionesha magamba ya risasi walizoshambuliwa.Picha: Reuters

Katika harakati hizo, jana Askofu Julius Kalu wa Dayosisi ya Mombasa alizuru eneo hilo ikiwa ni sehemu ya ujumbe huo wa amani. Ama kwa upande mwingine, viongozi wa kisiasa wa mkoa wa Pwani wameitwa mjini Nairobi wakati serikali ya Kenya ikifanya harakati za kumaliza mauaji kwenye eneo hilo.

Grace Kabogo amezungumza na Askofu Kalu kuhusiana na hali ilivyo kwa sasa kwenye eneo la Tana River. Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Grace Kabogo/Askofu Julius Kalu
Mhariri: Josephat Charo