1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Kosovo watishia kujitangazia uhuru

Siraj Kalyango10 Desemba 2007

Uhuru wake baado kizungumkuti

https://p.dw.com/p/CZnS
Hashim Thaci -kiongozi wa chama cha Democratic Party of Kosovo -PDK- akitoa ishara ya dole gumba baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa Kosovo mwezi Novemba 2007.Hata hivyo uhuru wa mkoa huo baado ni -suala nyeti ambalo limezigawanya nchi za Umoja wa Ulaya.Picha: picture-alliance/dpa

Viongozi wa Kosovo wanasema wataanza kampeini kali ya kuzungumzia kujitenga kwao kutoka Serbia.

Viongozi hao wanaungwa mkono na umoja wa Ulaya na matamshi yao yamekuja wakati mda uliotengwa na Umoja wa Mataifa kushughulikia suala hilo unafikia kikomo bila ya kupatikana kwa suluhisho.Suala la kujitenga kwa Kosovo kutoka kwa Serbia,baado hakujapata ufumbuzi, licha ya mda uliotolewa na Umoja wa Mataifa wa Disemba 10. Kosovo ni mkoa wa Serbia, lakini raia wake wengi ni wa ki Albania ambao walitendewa unyama na Serbia.Tangu mwaka wa 1999 mkoa huo umekuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa, kufuatia kuingilia kati kwa Umoja wa Ulaya wakati Serbia ilipokuwa inawasaka wapiganaji wa ki-Albania pamoja na wafuasi wao.Wapiganaji hao walitaka uhuru wa mkoa wao.

Kiongozi moja wa ki-Albania, Skender Hyseni, ambae ni mmoja wa ujumbe unaojadilia suala la kujitenga amesema kuwa kuazia leo Kosovo inaanza ushariano wa kina na washirika wao wa kimataifa, kwa lengo la kuratibu hatua za kujitangazia uhuru.Makundi ya vijana wa Kosovo wenye asili ya ki-Albania yaliandamana jumatu katika mji mkuu wa mkoa huo wa Pristina, kwa lengo la kuwahimiza viongozi wao kufuata mkondo wa kutaka uhuru wa mkoa huo.Hata hivyo kujitenga kwa mkoa huo sio tu umezusha sintofahamu miongoni mwa mataifa ya Ulaya lakini pia kuzusha mjadalakutoka kwa watu mbalimbali .Alfred de Zayas, ni mhadhiri wa masuala ya kiraia katika Chuo kikuu cha Havard…

’ serikali ya Urusi haitaunga mkono jambo hilo.Sioni Kosovo ikijiunga na Umoja wa Mataifa bila idhini ya urusi. Na pia sioni kama kuna umoja katika umoja wa Ulaya.Cyprus inahofia kuwa na jimbo huru kaskazini mwake, na Wahispania nao hawataki.Serbia nayo bila shaka haitaki eneo lingine linaloweza kuitwa la GALETIA likiwa huru,'

asema Zayas.

Ameongeza kuwa suala la uhuru wa Kosovo sio ufumbuzi pekee wa mgogoro huo.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, ameonya kile alichokiita, msururu wa matokeo,kutokana na hatua ya kuupa uhuru mkoa huo.lakini wenzake wa nchi za Umoja wa Ulaya wanasema wako karibu na kufikia msimamo wa pamoja wa kuitambua Kosovo kama nchi huru.Mjumbe wa Umoja wa Ulaya, ambae ni mwana diplomasia wa Kijerumani,Wolfgang Ischinger,yeye amenukuliwa akisema kuwa ikiwa Kosovo itajitenga Umoja wa Ulaya hautasita bali kuutambua.Mjumbe huyo akihojiwa na redio moja ya mjini Berlin-RBB-amesisitiza kuwa Umoja wa Ulaya utasisitiza kuwa Kosovo iliohuru inabidi itilie maanani sheria zinazoheshimu haki za waliowachache na pia kukubali katiba mpya ambayo tayari imetengenezwa.Hata hivyo amefafanua kuwa Kosovo haitakuwa huru kama vile Ujerumani ama Ufaransa bali itakuwa inaendelea kupewa kile alichokiita - ulinzi wa kimataifa.Amesema NATO itabakiza vikosi vyake huko. Nakuongeza kuwa huu utakuwa uhuru ambao unasimamiwa kimataifa.

Ischinger ambae aliongoza kamati iinayojumuisha Marekani,Umoja wa Ulaya na Urusi ikiwa na jukumu la kupata suluhu kati ya viongozi wa jimbo linalotaka kujitenga la Kosovo na viongozi wa Serbia.Anatarajiwa kuwafahamisha mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wa Brussels Ubelgiji kuwa ,mazungumzo kati ya wakuu wa Serbia na Kosovo hayakuzaa matunda yoyote.

Viongozi wa Kosovo wametishia kujitangazia uhuru ikiwa hakujapatikana muafaka wowote kuhusu dai lao la uhuru baada ya ile siku ya Disemba 10 .Serikali mpya ya Kosovo baado haijaundwa baada ya chama cha upinzani cha Hashim Thaci cha Democratic Party of Kosovo kushinda kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika mwezi jana. Nako mjini Belgrade, mji mkuu wa Serbia,Waziri mkuu Vojislav Kostunica amechelewesha uchaguzi wa rais,akisema utaweza kufunika mkakati wao wa kutaka kuibakiza Kosovo chini ya himaya yao.

Juhudi za Serbia za kuzuia uhuru wa Kosovo zinaungwa mkono na Russia.Aidha nchi zingine kama vile Slovakia,Ugiriki nazo zinasitasiata kuunga mkono uhuru wa mkoa huo zikihofia kuamsha hamasha za uhuru katika maeneo yao.