Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Martin Fayulu aliiomba Mahakama ya Katiba ya DRC kuyafuta matokeo ya uchaguzi

Martin Fayulu aliyakataa matokeo ya uchaguzi wa urais wa Desemba 30, 2018, ambapo alishika nafasi ya pili akiwa ameshindwa na Felix Tshisekedi, mgombea mwingine wa upinzani. Fayulu akafungua kesi kwenye Mahakama ya Katiba akiitaka iufute ushindi wa Tshisekedi. Lakini mahakama ikasema madai yake sio ''halali''. Fayulu alipata asilimia 34.8 ya kura, huku Tshisekedi akishinda kwa asilimia 38.57.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Maurice Kamto wa Cameroon ajitangaza mshindi

Maurice Kamto, mgombea wa upinzani wa muungano wa MRC na FDP, alijitangaza mshindi wa uchaguzi wa uraisi uliofanyika Jumapili ya Oktoba 7, 2018. Ni mmoja kati ya wagombea saba walioshindana na kiongozi wa muda mrefu wa Cameroon Paul Biya, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 36. "Ninamtaka Rais Biya ahakikishe kipindi cha amani cha mpito na kuepuka matukio yanayoweza kuwa mabaya," alisema Kamto.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Nelson Chamisa, 'rais halali' wa Zimbabwe

Kiongozi mdogo wa upinzani nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa, aliupinga ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi wa kwanza wa urais baada ya utawala wa Robert Mugabe uliofanyika Julai 30, 2018. Alijitangaza mshindi wa urais katika sherehe za kujiapisha.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Soumaila Cisse ayakataa matokeo nchini Mali

Soumaila Cisse wa Mali hakwenda mbali hadi kuandaa hafla ya kujiapisha, lakini alizungumzia kuhusu pengo la uongozi nchini Mali, baada ya mpinzani wake Ibrahim Boubacar Keita kuchukua madaraka. Agosti 20, Mahakama ya Katiba ilimtangaza Keita mshindi wa uchaguzi, baada ya kupata asilimia 67 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

'Rais wa wananchi' wa Kenya apeana mkono na mwenye mamlaka

Januari 20, 2018, Raila Odinga, mpinzani mkuu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, alijiapisha mwenyewe kama ''rais wa wananchi''. Alisusia marudio ya uchaguzi wa Oktoba 2017, baada ya kushinda kesi mahakamani kuhusu uhalali wa uchaguzi wa kwanza. Huku mazingira ya baada ya uchaguzi yakiwa ya wasiwasi, Machi 2018, Odinga na Kenyatta walitangaza kupeana mkono wa maridhiano na kusameheana.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Jean Ping: 'Nitatumia mamlaka mliyowekeza kwangu'

Miaka miwili baada ya uchaguzi wa urais Agosti 2016, kiongozi wa upinzani wa Gabon Jean Ping bado anaendelea kuonesha azma yake. Agosti 2018 alithibitisha nia yake ya kuendelea kupambana. Awali Ping alielekeza matumaini yake katika uchunguzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi, hata hivyo kesi hiyo ilifungwa. Haikukidhi vigezo vya uchunguzi.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Uganda's Besigye: Mpinzani wa muda mrefu

Februari 2016, Kizza Besigye aligombea urais kwa mara ya nne dhidi ya kiongozi wa muda mrefu wa Uganda, Yoweri Museveni. Wakati Museveni alipotangazwa mshindi, Besigye alijiapisha mwenyewe katika sherehe mbadala. Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini, lakini aliachiwa huru wiki chache baadae.

Viongozi wa upinzani Afrika waliojitangazia ushindi mapema

Etienne Tshisekedi: 'Mshindi' wa mara mbili wa DRC

Mwaka 2006 na 2011, Etienne Tshisekedi, kiongozi wa chama cha UDPS katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, alidai kumshinda Rais Joseph Kabila. Alionekana kama mmoja wa wapinzani wakuu wa Kabila, akiwa na matumaini ya kugombea katika uchaguzi mwingine. Alifariki mwaka 2017 baada ya kuugua na baada ya hapo, mtoto wake Felix alichukua uongozi wa chama.

Kuna historia ndefu ya wagombea wa upinzani Afrika ambao wamejitangaza kushinda katika uchaguzi. Wengi waliyapinga matokeo mahakamani, wakidai kwamba uchaguzi ulikuwa wa udanganyifu. Hawa hapa ni wachache tu.

 

 

Zaidi katika Media Center

Tufuatilie