1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vipi Rwanda ilivyopokea hukumu ya Theoneste Bagosora

18 Desemba 2008

Jumuiya ya watu walionusurika mauaji ya kuangamiza jamii nchini Rwanda ijulikanayo kama IBUKA, imefurahia hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda.

https://p.dw.com/p/GJEB
Rwanda imefurahia hukumu ya Theoneste BagosoraPicha: AP

Wasema hukumu hiyo ni onyo kwa wengine ambao wangethubutu kutumia madaraka yao kukanyaga haki za watu wengine. Hata hivyo katibu mkuu wa jumuiya hiyo Benoit( soma Benua) Kaboyi, anasema hawakuridhika na hukumu kwa mtuhumiwa mwingine Kabiligi Gratian, ambaye mahakama hiyo haikumkuta na hatia.

Zaidi anayo Daniel Gakuba kutoka Kigali.