1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Virusi vya ugonjwa wa miguu na midomo vimetokea maabara

P.Martin5 Agosti 2007

Wizara ya mazingira ya Uingereza imesema,virusi vya ugonjwa wa miguu na midomo vilivyogunduliwa katika ngombe wa shamba moja kusini mwa nchi, vimefanana na vile vinavyofanyiwa utafiti katika kampuni moja ya Kimarekani ilio jirani.

https://p.dw.com/p/CB2D
Maafisa wa polisi wakizuia watu na magari kuingia barabara inayopita karibu na shamba la mifugo iliyoambukizwa,kusini mwa Uingereza
Maafisa wa polisi wakizuia watu na magari kuingia barabara inayopita karibu na shamba la mifugo iliyoambukizwa,kusini mwa UingerezaPicha: AP

Kwa maoni ya wataalamu,virusi hivyo vimetokea maabara ya kampuni hiyo na kuwaambukiza ngombe katika shamba lililo umbali wa kiasi ya kilomita sita.

Serikali ya Uingereza,imeamaua kwa hiyari kupiga marufuku usafirishaji wa mifugo na bidhaa za wanyama.Hali ya wasiwasi pia imeufanya Umoja wa Ulaya,kupiga marufuku kuagizia mifugo kutoka Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema, serikali itachukua hatua za haraka kudhibiti ugonjwa huo.

Mripuko wa ugonjwa wa miguu na midomo katika mwaka 2001 ulipelekea kuua mifugo milioni 7 na uliathiri vibaya sana sekta za kilimo na utalii.