1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita-Gaza-Mashambulizi makali katika barabara za Gaza.

Eric Kalume Ponda13 Januari 2009

Kumetokea mashambulizi makali katika barabara za mji wa Gaza wakati wanajeshi wa Israel walipoimarisha oparesheni yao na kuingia katika eneo lenye idadi kubwa ya watu katika mji huo.

https://p.dw.com/p/GXC3
Mabomu ya fosiforasi yanayodaiwa kutumiwa na wanajeshi wa IsraelPicha: AP


Mashambulizi hayo yameendelea usiku kucha baada ya Israel kutangaza kwamba, sasa oparesheni hiyo inaingia awamu yake ya tatu na kuiwaita wanajeshi zaidi wa akiba.


Hali kadhalika wanajeshi wa Israel wanaoshika doria katika eneo la Joradn walishambuliwa mapema leo katika eneo hilo ingawa bado haijabanika nani alihusika na shambulio hilo.


Wanajeshi wa Israel wakitumia vifaru vya kijeshi sasa yaripotiwa wako hatua chache tu kutoka vitongoji vya mji wa Gaza kufuatia mashambulizi hayo ya usiku kucha.


Ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi dhidi ya vituo 60 vinavyodaiwa kutumiwa na wafuasi wa Hamas kurushia makombora ya Maroketi katika ardhi yake.


Mashambulizi hayo yametokea katika kitongoji cha Tal Al Hawa na Sheikh Anjlin ambako watu 12 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.


Wafuasi wa chama cha Hamas walijibu mashambulizi hayo kwa kurusha makomora ya maroketi ndani ya Israel huku wakiwashambulia wanajeshi hao kwa mabomu yaliyotegwa kando ya barabara na mizinga.


Vingora vilisikika katika miji ya kusini mwa Israel ya Ashklone ingawa hakuna habari zilizotolewa mara moja kuhusu majeruhi katika upande wa Israel.


Kuna habari kwamba wanajeshi wa Israel wamekuwa wakitumia mabomu yaliyotengenezwa na kemikali aina ya Fosiforasi licha ya kukanusha madai hao.


Hii si mara ya kwanza madai hayo kutolewa kwani itakumbukwa kwamba mapema wiki hii baraza la kutetea haki za binadamu la umoja wa mataifa lilitoa taarifa kwamba Israel inatumia aina hiyo ya mabumu na hivyon basi kuikuka maazimio ya Umoja wa mataifa.

Mkaazi mmoja wa eneo la Najar Bw Yabilia alisema kuwa watu wengi wameteketea kufuatia mashambulilizi ya kutumia aina hiyo ya Mabomu mkaazi mmoja wa mji huo .`` Mashambulizi haya ni makali na huwezi kuamini kwani sasa wanajeshi wa Israel wanatumia mabomu ya kemikali aina ya fosiforasi.Kama unavyojua mabomu hayo ni hatari na yamewaua watu wengi sana katika eneo hili Pia wamefanya mashambulizi makali katika eneo la Najar na mashariki mwa Gaza ambako watu wengi wameuliwa. Mabomu haya ni hatari na unaweza kufikiria jinsi yalivyoteketeza watu´´


Hata hivyo dai hilo limepingwa vikali na Israel ikisema kuwa kamwe haiwezi kutumia silaha ambayo zinakiuka maazimio ya Umoja wa mataifa. Msemaji wa jeshi la Israel Avital Liebovich alisema kuwa Israel itaendelea na mashambulizi hayo katika hatua ya kukomesha kabisha mashambulizi ya marokoeti kutoka kwa Hamas lakini haiwezi kutumia silaha ambayo haziambatani na maazimio ya Umoja wa mataifa.Liebovich alisema. ``Silaha zote zinazotumiwa na Israel zinambatana na viwango na sheria za kimataifa. Israel haiwezi kutoa habari zaidi kuhusu ni aina gani ya silaha inazotumia katika oparesheni hii´´.


Mashambulizi hayo yameendelea licha ya wito wa jamii ya kimataifa kutaka kukomeshwa kwa vita hivyo. Israel na chama cha Hamas vimekataa azimio la Umoja wa mataifa kutaka kukomeshwa mara moja kwa vita hivyo, na sasa matumaini yaliyosalia ni kwa mpango wa amani unaoongozwa na Misri.


Wajumbe wa chama cha Hamas wamekuwa mjini Cairo kuhudhuria mashauriano hayo ingawa walisema kuwa pendekezo lililotolewa kuhusu kusitishwa kwa mapigano linapasa kufanyiwa marekebisho kabla ya kukubaliwa na wafuasi wa Hamas.


Kiongozi wa chama cha Hamas Ismail Haniya alisema kuwa licha ya mashambilio hayo Hamas itaibuka mshindi kwenye vita hivyo.


Zaidi ya Wapalestina 800 wameuwa na wengine wasiopungua 3000 kujeruhiwa tangu vita hivyo vianze disemba 27.