1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya Kongo: Pande zote zinazohusika zinapaswa kufahamu umuhimu wa amani.

17 Novemba 2008

Jamii ya kimataifa imechangia mabilioni ya fedha kwa ajili hiyo

https://p.dw.com/p/FwNA

Tangu yalipoanza mapigano mapya Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwezi Agosti, kiasi ya watu 250.00 mashariki mwa nchi hiyo wamelazimika kuwa wakimbizi.Kiongozi wa waasi Laurent Nkunda anawaongoza waasi wa Kitutsi wanaopigana na jeshi la taifa. Mapigano hayo yamechukua pia sura ya kikabila ya uhasama kati ya Wahutu na Watutsi.

Nchi hiyo ilikua na habari za matumaini, pale baada ya vita vya miaka kadhaa ,ulipofikiwa hatimae mkataba wa amani 2002 na kufuatiwa na uchaguzi ambao kwa kiwango kikubwa uliandaliwa vizuri 2006. Nini yalikua matokeo : Kupatikana utawala halali wa kisiasa katika mji mkuu Kinshasa.

Hatimae yalitokeza matumaini ya amani katika taifa hilo ambalo ni moyo wa bara la Afrika, na kuwa mahala kuwekeza jumuiya ya kimataifa. Kuna ujumbe mkubwa kabisa wa Umoja wa mataifa ukiwa na wanajeshi 17.000 wa kulinda amani na Umoja wa Ulaya ulituma kikosi cha kijeshi kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi huo.

Sasa matumaini yameingia dosari:Vita vimerudi tena upya mashariki mwa nchi hiyo katika mkoa wa Kivu Kaskazini na halikadhalika mbali zaidi katika upande wa kaskazini katika wilaya ya Ituri kwenye mpaka na Uganda na pia katika mpaka na Sudan. Waakazi maeneo hayo wamekua wahanga wa vita tangu miaka ya 90.

Upande wa mashariki mgogoro huu ni wa kutatanisha zaidi ukiwa ni kati ya wenyewe kwa wenyewe: Majeshi ya serikali dhidi ya Jenerali Mtutsi na kiongozi wa waasi Nkunda, wanamgambo nao dhidi ya raia waliosimama kidete. Angola nayo imetangaza kuwa itatuma wanajeshi kuisaidia serikali ya Kongo.

Pengine Kongo ni mfano mzuri zaidi panapohusika na suala la uchaguzi, kwamba kunahitajika udhibiti wa kisiasa na mikakati inayoandamana na utawala kutibiwa macho.Tabaka ya kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo lakini inaelewa vyengine: Ushindi kwao ulikua sawa na kufungua milango ya kuchotwa mali asili hali inayoandamnana na uhasama kati ya Wahutu na Watutsi mashariki mwa nchi hiyo.

Kutokana na hayo Kongo yenye utajiri mkubwa wa mali asili barani Afrika, imepoteza nafasi ya kudhibiti vyema uongozi, kiuchumi na kisiasa.Jamii ya kimataifa imetumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya amani nchini Kongo na haiana budi kuhakikisha kwamba amani haivurugwi sio na Kinshasa wala wanamgambo katika kanda hiyo na pia kuhakikisha wazi kwamba mataifa jirani nayo Rwanda, Uganda na Angola yanawajibu wa kuhakikisha amani inadumu nchini Kongo.

Mtu unajiuliza kwanini viongozi wa nchi za kiafrika walikutana kuujadili mgogoro huo wa Kongo mjini Nairobi na kumaliza na kuondoka kwa maneno matupu tu kwamba wote wanataka kuona amani inapatikana, wakati huko Goma, Beni au Butemba matumizi ya nguvu na mauaji yanaendelea ? Haya yanasikitisha na hali hii haiendani na sura ya mageuzi na demokrasia ambayo Marais wa Afrika wanataka kukuijenga.