1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vita vya mtandaoni vyakaribia

Sekione Kitojo1 Julai 2010

Hadi hivi sasa kumefanyika vita vya ardhini, majini na angani. Sasa kunakuja aina nyingine kabisa ya vita, vita vya mawasiliano ya mtandaoni.

https://p.dw.com/p/O8Vr
Mkutano wa mizozo ya mtandaoni uliofanyika nchini Estonia hivi karibuni .Picha: DW

Hadi hivi sasa kumefanyika vita vya ardhini, majini na angani. Sasa kunakuja aina nyingine kabisa ya vita. Vita vya mawasiliano mtandaoni. Hali inayozidi kukua ya kutegemea zaidi miundo mbinu ya teknolojia ya mawasiliano inaelekeza katika hali isiyo salama ya kushambuliwa mawasiliano hayo. Majeshi pamoja na idara za usalama yamekwisha iona hali hiyo kwa muda mrefu na wameanza kulishughulikia suala hilo kikamilifu.

Kwa kifupi, ufanisi wa kiuchumi wa Marekani katika karne ya 21, utategemea sana, usalama wa mawasiliano ya mtandao.

Ni ukweli usiokanika kutoka kwa rais wa Marekani Barack Obama. Katika mwezi wa Mei , mwaka 2009 alikuwa rais wa kwanza wa Marekani kuweza kuzungumzia katika hotuba yake kuhusu usalama wa mawasiliano ya mtandao. Obama amesisitiza hatari ya kutegemea mtandao wa kompyuta, mafuta na gesi, umeme na maji, vitu ambavyo upatikanaji wake unaweza kuvurugwa pamoja na usalama wa safari za ndege ulivyo katika hatari. Kutokana na kukabiliwa na hali hii isiyo salama rais Obama anataka mfumo wa kuulinda mtandao.

Ni kweli kwamba katika dunia ya leo vitendo vya ugaidi vinaweza kutokea , sio tu kwa watu wachache wenye imani kali wanaovaa mikanda ya kujilipua, lakini kwa kugusa vitufe vichache tu katika kompyuta. Silaha ya amaangamizi.

Mwaka mmoja baada ya hotuba hii, tarehe 21 Mei 2010 Jenerali Keith Alexander alitunukiwa nyota yake ya nne. Mkuu wa idara ya usalama wa ndani, NSA, na pia alipokea wadhifa wa kamanda wa idara ya mawasiliano katika mtandao. Idara ya NSA inakuwa idara kuu ya ujasusi na yenye mamlaka katika Marekani. NSA ni mwajiri mkuu duniani hivi sasa wa wataalamu wa hesabu. Kutokea katika makao yake makuu mjini Fort Mead, idara hii inaangalia mawasiliano yote ya mtandaoni duniani kote, kuchunguza na kutambua maandishi ya siri, pamoja na kuyatathmini. wakati Keith Alexander alipoanza kazi rasmi kama mkuu wa kamandi ya mawasiliano ya mtandaoni, hapo Juni 3, aliielezea hali kuwa ya kutisha. Mara milioni sita kila siku, unashambuliwa mfumo wa mtandao wa wizara ya ulinzi, anasema Alexander na hali hiyo inaendelea.

Utajiri wa Marekani na nguvu zake unaifanya nchi hii kuwa lengo la mashambulizi katika mtandao wa mawasiliano. Na moja kati ya nguzo za nguvu zetu, jeshi letu, iko katika hatari, huenda katika kiwango cha juu kabisa. Jeshi letu linategemea mtandao wake ili kufanya udhibiti wa uongozi, mawasiliano, ujasusi, uendeshaji na usafirishaji wa vitu mbali mbali. Katika idara ya ulinzi tuna zaidi ya mashine milioni 7 za kuzilinda ambazo zimeunganishwa katika karibu mitandao 15,000.

Mwaka mmoja uliopita waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates alisema kuwa idadi ya wataalamu wa usalama wa mtandao wa kompyuta waongezwe mara nne. Na hii sio tu kwa ajili ya kujilinda na kulinda mfumo wa nchi hiyo tu. Mtaalamu wa masuala ya kompyuta nchini Marekani Herbert Lin , anazungumzia pia kuhusiana baadhi ya mashambulizi haya. Anasema kuwa mataifa kadha yanajaribu kujilinda na pia kushambulia katika mtandao. Lakini mjadala wa wazi unatuwama hususan katika viwango vya kujilinda. Ni watu wachache sana wameweza kuzungumzia kuhusu viwango vya mashambulio, lakini hii ni sehemu muhimu ya sera za usalama katika mtandao.

Mwandishi : Matthias von Hein / ZR / Sekione Kitojo.

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

Audio-Link: