1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vlabu vyaendekeza tamaa ya pesa mbele ya Corona

Iddi Ssessanga
11 Machi 2020

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia vilabu vya soka vyenye tamaa ya pesa, mabadiliko ya katiba nchini Urusi, chuki na vurugu Ujerumani na swali la kansela katika chama cha SPD.

https://p.dw.com/p/3ZCuZ
Bundespräsident Steinmeier besucht Zwickau
Picha: picture-alliance/dpa/S. Kahnert

Mhariri wa gazeti la Schwäbische Zeitung la mjini Ravensburg ameandika juu ya tamaa ya vilabu vya soka nchini Ujerumani.

Mhariri huyo anasema ukweli kwamba soka imegeuka kuwa dini mbadala nchini Ujerumani unaonekana katika namna unavyoshughulikia mripuko wa virusi vya corona.

Wakati maonesho mbalimbali, matukio madogo na makubwa ya kimichezo na kitadamu yamefutwa, kutokana na virusi hivyo, soka imeendelea ili kuhakikisha hawapotezi mamilioni ya mapato na hakuna aliweza kuwazuwia hadi waziri wa afya Jens Spahn alipoingilia siku ya Jumapili na kutaka matukio yote yenye mikusanyiko mikubwa yasitishwe.

Vilabu vya Ligi ya Shirikisho la Ujerumani - DFL vina utajiri wa kutosha kuweza kuhimili mapumziko ya kati ya wiki mbili hadi nne bila mashabiki. Hili ni muhimu kwa Ujerumani lakini DFL inakataa. Inaangalia pesa zaidi kwa gharama ya afya ya watu. Shirkisho hilo linapaswa kuacha kuchezea kifo.

Mahriri wa gazeti la Volksstimme ameandika juu ya mapendezo ya mabaliko ya katiba nchini Urusi ambayo huenda yakampa rais wa nchi hico Vladmir Putin nafasi ya kutawala maisha, iwapo ukomo wa mihula utaondolewa.

Borussia Mönchengladbach Stadion Borussia-Park
Uwanja wa klabu ya Borrusia Mönchengladbach wa Borrusia-Park.Picha: imago images/Nordphoto/Ewert

Mhariri huyo anasema Vladmir Putin anajihakikishia kuwa mtawala pekee baada ya muhula wake kumalizika hapo 2024. Hiyo siyo habari mbari mbaya kwa mataifa ya magharibi, inamaanisha kuwa iwapo mfalme huyo atakuwa na afya njema, kutakuwa na miaka kadhaa ya utulivu nchini Urusi. Putin ni sehemu ya mfumo ambao unaofanyakazi tu akiwepo madarakani.

Licha ya matatizo yake yote, anaendelea kuwa mtu anayetabirika na kuondoka kwake kunaweza kusababisha mzozo mkubwa nchini Urusi. Mataifa ya Magharibi yanaweza kuwa na matumani tu kwamba jamii na uchumi wa Urusi vinaendelea kustawi licha ya mfalme Putin. Urusi yenye malighafi na silaha kamwe haiwezi kuwa demokrasia.

Chuki na vurugu Ujerumani

Rais wa Ujerumani Frank-Walter steinmeier amewatolea mwito wale aliowaita wengi waliokimya kujitokeza na kupaza sauti na kukabiliana na chuki na vurugu nchini Ujerumani, kufuatia kuongeza kwa vitendo vya chuki na vurugu vinavyochochewa na wafuasi wa itikadi kali za mrengo wa kulia.

Mhariri wa gazeti la Ostfriesen-Zeitung anasesema katika muktadha huu, miito kwa raia inaweza kuwa na athari tu katika hatua ya pili au ya tatu.

Hatua ya kwanza inapaswa kuwa mapambano ya serikali dhidi ya vinamasi vya itikadi kali za mrengo wa kulia - katika ufahamu mgumu kwamba watu wengi wanaowachagua wanasiasa wa siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wanajua vizuri kile wanachokifanya.

Deutschland, Berlin: Altkanzler Gerhard Schröder gibt ein Interview
Kansel wa zamani wa Ujerumani Gerhard Schröder.Picha: Reuters/F. Bensch

Mjadala kuhusu mgombea ukansela wa SPD

Mjadala kuhusu suala la nani atakuwa mgombea wa nafasi ya kanesele kupitia chama cha Social Democratic SPD, umeanzishwa na kansela wa zamani Gerhard Schröder.

Mhariri wa gazeti la Frankenpost anasema Gerhard Schröder ameifanyia hisani SPD kwa kuanzisha mjadala huo, ingawa hakuingilia katika kutokana na mapenzi ya dhati kwa chama, bali kutokana kutopenda kwake viongozi wawili wa chama hicho Saskia Esken na Norbert Walter-Borjans.

Kwa usahihi, kansela huyo wa zamani haoni kati ya wawili hao anaestahili kuwa kansela.Miongoni mwa Wasocial Democrat watano ambao anawapendelea, Franziska Giffey anashika nafasi ya usoni.

Anfanya kazi nzuri kama waziri wa masuala ya familia, anazungumza lugha ya raia na anasimamia kwadhati demokrasia ya kijamii. Na juu ya yote anaonekana kijana zaidi kuliko wagombea wa chama tawala cha CDU.

Chanzo: Magazeti ya Ujerumani