1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyombo vya habari na mustakabali wa lugha ya Kiswahili

2 Juni 2015

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuitangaza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili. Lakini kuna wasiwasi uliojitokeza kwamba vyombo hivi vimeanza kuiharibu lugha hiyo.

https://p.dw.com/p/1FajX
Bayreuth - 28. Swahili Kolloquium
Mohammed Khelef (kulia) wakati alipomhoji Ken Walibora mjini BayreuthPicha: DW/M. Khelef

Ingawa kuongezeka kwa vituo vya redio vinavyotumia lugha ya Kiswahili kwenye maeneo ya Afrika Mashariki kulitazamiwa kuwe neema kwa lugha hiyo, wasomi na wataalamu wa lugha wanahofia kwamba aina ya Kiswahili kinachotumiwa kwenye vituo hivyo vya redio kinakwamisha maendeleo halisi ya Kiswahili.

Mohammed Khelef alihudhuria Kongamano la 28 la Kiswahili lililofanyika katika mji wa kusini mwa Ujerumani, Bayreuth, na kuzungumza na Profesa Ken Walibora kutoka Kenya, ambaye kwanza anaelezea kiini cha wasiwasi alionao juu ya mustakabali wa lugha ya Kiswahili.

Kusikiliza mahojiano haya bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Josephat Charo