1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vyombo vya habari vyazuiwa kuzungumzia siasa Kameroon

26 Septemba 2013

Wakameroon wanatarajiwa kuwachagua wabunge wao 180 pamoja na viongozi wa serikali za mitaa katika uchaguzi utakaohusisha majimbo 360 Jumatatu ijayo Septemba 30.

https://p.dw.com/p/19ofz
Supporters of Presidential candidate of Social Democratic Front party, Ni John Fru Ndi, attend an election rally in Yaounde, Cameroon, Saturday, Oct. 8. 2011. Cameroon goes to the polls Sunday in the final round of presidential elections. (Foto:Sunday Alamba/AP/dapd)
Uchaguzi nchini CameroonPicha: dapd

Wakati kampeni zinaanza kupamba moto , serikali ya Cameroon imesitisha vipindi 130 vya vyombo vya habari na mijadala ambayo inahusisha siasa katika vituo vya radio na televisheni nchini humo.

Waandishi habari wanasema kuwa hawawezi kukiuka amri hiyo kwa kuhofia vituo vyao kufungwa. Hii inakuja baada ya kufungwa na kusitishwa kufanyakazi kwa radio , Televisheni na magazeti 11.

George Etame mwenye umri wa miaka 45 anasafisha banda lake la kuku katika mji wa Sao nje kidogo ya mji wa Yaounde, mji mkuu wa Cameroon. Kwa muda wa siku 10 sasa, hajaweza kusikiliza kipindi chake akipendacho sana katika radio ambacho kinajadili masuala ya siasa katika lugha ya kwao ya Kiewondo.

A picture taken on March 16, 2009 of the Yaounde main market. Kidnappers who seized seven members of a French family, including four young children, in Cameroon, have taken them across the border into Nigeria, Cameroon's government has said on February 20, 2013. The family -- a couple, their children aged five, eight, 10 and 12 and an uncle -- were snatched by six gunmen on three motorbikes on February 19. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO (Photo credit should read ISSOUF SANOGO/AFP/Getty Images)
Sehemu ya jiji la YaoundePicha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

"Kila mara nasikiliza vipindi vya radio vinavyohusu masuala ya siasa. Lakini kwa muda sasa , kila nikifungulia radio, nasikia muziki tu. Sijui kwanini".

Etame George anasema ana alikuwa akitegemea kipindi cha radio kumpa habari juu ya wanasiasa wanaoshiriki katika uchaguzi wa mabaraza ya miji pamoja na wabunge pamoja na sera zao.

"Nataka kupiga kura. Lakini sifahamu mtu wa kumpigia kura kwasababu hakuna mwanasiasa aliyefika hapa kutufahamisha kile atakachokifanya iwapo atachaguliwa".

Ufugaji wa kiwango kidogo wa kuku ni miongoni mwa Wacameroon wengi ambao wamekosa mipango ambayo inahusiana na masuala ya kisiasa kufuatia kusitishwa kwa vipindi kama hivyo katika redio zote za umma na za binafsi pamoja na vituo vya televisheni nchini humo.

Supporters of Ni John Fru Ndi Social Democratic Front, Presidential candidate, attend an election campaign rally in Yaounde, Cameroon, Saturday, Oct. 8. 2011. Cameroon goes to the polls Sunday in the final round of presidential elections. (Foto:Sunday Alamba/AP/dapd)
Wafuasi wa chama cha siasa nchini CameroonPicha: dapd

Kituo cha taifa cha matangazo cha CRTV kimekuwa mara kadha kikiwakumbusha wananchi juu ya kusitishwa na kile kinachotarajiwa dhidi ya vyombo vya habari vitakavyopinga amri hiyo.

Waziri wa mawasiliano amesitisha utengenezaji wa vipindi vyote vya kisiasa wakati nchi hiyo ikijitayarisha na uchaguzi wa mabaraza ya miji na wabunge katika uchaguzi wa Septemba 30.

Mkaguzi mkuu katika wizara ya mawasiliano nchini Cameroon , Dr. Felix Zogo amesema kuwa vipindi hivyo vimezuiwa katika juhudi ya kulinda vyama vya siasa ambavyo havina uwezo wa kupata nafasi katika vyombo vya habari kuweza kufunikwa katika kampeni na vyama vyenye uwezo wa kupata nafasi katika vyombo vya habari vinavyoendeshwa na vyama hivyo.

Cameroon president Paul Biya waves as he leaves the Elysee Palace following a meeting with French president at on January 30, 2013 in Paris. Biya is in Paris on a working visit to meet French business leaders. AFP PHOTO / PATRICK KOVARIK (Photo credit should read PATRICK KOVARIK/AFP/Getty Images)
Rais wa Cameroon Paul BiyaPicha: Patrick Kovarik/AFP/Getty Images

"Tuna vyama 43 vya siasa vinavyopambana kwa hiyo mwandishi habari anakuwa na wapinzani 20 mahali fulani ama studio kuzungumza nao. Ni vigumu na ndio sababu ilikuwa bora kusitisha vipindi vyote ambavyo vinashughulika na masuala ya siasa ili kuhakikisha usawa".

Kumekuwa na maelezo tofauti kutoka kwa wanahabari nchini Cameroon. Serge Pouth , mwandishi habari wa shirika la utangazaji la taifa ambaye anatangaza vipindi vya siasa ana mawazo kuwa waandishi habari wanapaswa kufanyakazi kitaalamu zaidi katika kazi yao ili kuepuka hali kama hizo.

Mwandishi: Moki Kindzeka / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Josephat Charo