1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji Ukraine wavamia ofisi za serikali

2 Desemba 2013

Takribani waandamanaji 1,000 nchini Ukraine wamevamia makao makuu ya ofisi za serikali na kwenye mitaa mbali mbali mjini KIEV leo na kuathiri shughuli za serikali.

https://p.dw.com/p/1ARah
Waandamanaji Ukraine wakiwa katika mitaa mbali mbali.
Waandamanaji Ukraine wakiwa katika mitaa mbali mbali.Picha: Reuters

Waandamanaji hao pia walizuia wafanyakazi kuendelea na shughuli zao wakishinikiza msukumo mpya kudai rais Viktor Yanukovich ajiuzulu kutokana na mzozo wa uhusiano na Umoja wa Ulaya.

Maadamano hayo yamefutia mkaubliano ya wananchi kuitiisha maandamano ya nchi nzima , ambapo walifunga njia kuu ya kuingilia kwenye majengo ya serikali huku wakiwa wamebeba mabanko yenye jumbe mbali mbali.

Msemaji wa makamu wa rais wa nchi hiyo, Mykola Azarov amesema kuwa wafanyakazi wameshindwa kuingia ofisini, huku wakifanya juhudi za kuzungumza na waandamanaji hao kuwaruhusu wafanyakazi kuingia ofisini, na kuwaeleza kuwa, rais Azarov alikuwa hajawasili kazini.

Maandamano hayo yalilenga majengo ya serikali baada ya maadamano ya upinzani yaliyohusisha takribani watu 350,000 jana, katika mji mkuu wa Ukraine, KIEV na kusababisha vurugu baina ya polisi na waandamanaji hao.

Rais Viktor Yanukovich hajazungumzia chochote

Rais Viktor Yanukovich hajazungumzia chochote kufuatia vurugu zinazotokana na maandamano hayo, huku kukiwa na taarifa kwamba anatarajia kuondoka nchini humo kesho kwa ziara ya kikazi nchini China.

Waandamanaji Ukraine wakiwa na mabanko.
Waandamanaji Ukraine wakiwa na mabanko.Picha: Reuters

Taarifa zinasema kuwa wafanyakazi katika ofisi yake waliendelea na shughuli zao kama kawaida, lakini walikataa kuzungumzia wapi rais huyo alikuwepo.

Upinzani nchini humo unashinikiza rais Yanukovich ajiuzulu, kufuatia rais huyo kukataa kutia saini makubaliano ya kisiasa na kibiashara pamoja na Umoja wa Ulaya.

Watu kadhaa walijeruhiwa mwishoni mwa wiki baada ya polisi wa kuzuia ghasia kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia nguvu ambapo kikundi cha waandamanaji waliojiziba nyuso walishambuliana na polisi na kuharibu sanamu ya picha ya mwanzilishi wa Umoja wa Kisovieti, Vladimir Lenin.

Hata hivyo Benki ya Taifa ya nchi hiyo ambayo ipo karibu na majengo ya serikali imeendela na kazi zake, ingawa waandamanaji walisambaa kati kati ya mji wa KIEV na hivyo wafanyakazi kutangazia kubakia nyumbani.

Migomo ndani ya ofisi za serikali

Kwa mujibu wa waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Yuri Lutsenko ambaye sasa ni miongoni mwa viongozi wakuu wa upinziani amesema kinachoendelea sasa katika ofisi mbali mbali za serikali ni migomo.

Hata hivyo mfanyakazi mmoja anayefanya upande wa matangazo amesema kwa upande wake ameamua kwenda kazini, na kwamba ni matumaini yake kuwa wakuu wake hawatamfukuza kazi kwani kitengo chake kinaendelea na kazi na kushinikiza kwamba wengine hawakubali kuandamana kutokana na majukumu ya kulisha familia.

Askari polisi wakizuia maandamano.
Askari polisi wakizuia maandamano.Picha: Reuters

Mfanyakazi mmoja wa serikali amesema kuwa alifikia ofisini kwake na kujaribu kuingia ndani lakini alizuiwa baada ya kuarifiwa arudi yumbani na kusubiri maelekezo zaidi.

Mwandishi: Flora Nzema/RTRE

Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman