1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wameshambuliwa nchini Yemen

30 Mei 2011

Watu 4 wameuawa na wengine 90 wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji nchini Yemen

https://p.dw.com/p/11QPF
Mapigano yameenea nje ya mji mkuu Sana'aPicha: AP

Vikosi vya usalama nchini Yemen viliwashambulia waandamanaji katika mji uliopo kusini,Taiz hapo jana na kuwaua watu 4 na kuwajeruhi wengine 90.

Jemen Demo Soldaten
Wanajeshi wa Yemen waliosaliti amri na kujiunga na waandamanajiPicha: AP

Maafisa katika hospitali wamesema vikosi hivyo vya usalama vinavyomuunga mkono rais Ali Abdullah Saleh, viliwashambulia kwa silaha waandamanaji.

Mapema hapo jana upinzani nchini humo na waziri wa zamani wa ulinzi aliyejiuzulu serikalini, jenerali Abdullah Ali Aleiwa, walimlaumu rais huyo kwa kuuruhusu mji uliopo kusini, Zinjibar, kuanguka mikononi mwa kundi la kigaidi la Al Qaeda, ili ayashawishi mataifa ya magharibi yamruhusu asalie madarakani.

Mwandishi:Maryam Abdalla/Afp/Rtre.