1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waandamanaji wawafurumusha wanamgambo Benghazi

22 Septemba 2012

Walibya waliyochoshwa na ushawishi wa makundi ya wanamgambo mjini Benghazi walivamia kituo cha kundi la wanamgambo na brigedi ya waasi wa zamani na kusababisha mtifuano uliyosababisha vifo vya watu wasiyopungua wanne .

https://p.dw.com/p/16Cbb
Waandamanaji mjini Benghazi, Libya.
Waandamanaji mjini Benghazi, LibyaPicha: Reuters

Mamia ya wakaazi walioandamana Ijumaa hadi usiki wakuamkia jumamosi walivamia makao makuu ya brigedi ya Raf Allah al-Sahati iliyoko katika shamba moja mkoani Hawari, kilomita 15 kutoka Benghazi, ambapo watu wengine 40 walijeruhiwa katika mapigano baina ya waandamanaji hao na kundi hilo la Raf Allah, ambalo liko chini ya wizara ya Ulinzi ya Libya. Pande mbili zilishambuliana kwa kutumia maroketi na silaha nyingine ndogondogo kwa muda wa masaa mawili, kabla ya kundi hilo kuamua kuondoka katika kambi yake, na kusafisha njia kwa waporaji kuiba silaha na vitu vingine.

Mwandishi wa habari wa shirika la Ufaransa, AFP aliyekuwepo katika tukio hilo alisema wavamizi hao walitia moto jengo moja na kuanza kupora maghala ambapo walichukua vifaa vya umeme, silaha na risasi. Mapema mamia ya waandamanaji walivamia walikivamia kituo cha kundila wanamgambo wenye msimamo mkali la Ansar al-Sharia na kulilaazimisha kukimbia kabla ya kukitia moto kituo chake. Wanachama wa kundi hilo walipiga risasi hewani kabla ya kulaazimishwa kuondoka.

Gari la ofisi ya uwakishi ya Marekani mjini Benghazi likiteketea kwa moto baada ya uvamizi wa ofisi hiyo Septemba 11.
Gari la ofisi ya uwakishi ya Marekani mjini Benghazi likiteketea kwa moto baada ya uvamizi wa ofisi hiyo Septemba 11.Picha: picture-alliance/dpa

Vurugu zilikuja baada ya takriban wakaazi 30,000 wa mji huo ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Libya, kufanya maandamano mapema siku ya Ijumaa kupinga kuongezeka kwa ushawishi wa makundi ya wanamgambo katikamji huo, ambao wakosoaji wanasema wamejiweka juu ya sheria. Serikali ya Libya ilionya dhidi ya kufanya vurugu na kuwataka waandamanaji watofautishe kati ya makundi haramu na yale yaliyoko chini ya udhibiti wa serikali. Rais wa bunge la Libya Mohamed al-Megaryef alikaribisha hatua hiyo ya raia kupinga makundi haramu yenye silaha,lakini aliwataka waandamanaji kuondoka katika vituo vya brigedi za serikali zikiwemo Raf Allah al-Sahati, February 17 na Shielf Libya.

Waziri aonye juu ya moli katika maandamano

Waziri wa mambo ya ndani Fawzi Abdelali alionya kuwa kulikuwepo na watu waliojipenyeza katika maandamano hayona kuongeza kuwa baadhi yao walikuwa maafisa wa vikosi vya uslama waliyolenga kuchochea vurugu. Maandamano ya amani baada swalaya Ijumaa yalifunika mkutano uliyoitishwa na waislamu wa salafi na kuhudhuriwa na mamia waliokasirishwa na filamu na vikaragosi vinavyomdhihaki Mtume Muhammad.

"Hapana kwa makundi yenye silaha" na ndiyo kwa jeshi la Libya, lilisomeka bango moja lililobebwa na waandamanaji waliyokuwa karibu na Hoteli ya Tibesti, kabla ya kuelekea uwanja wa Al-Kish karibu na kambi yenye iliyo na brigedi kadhaa. Mabango hayo yalikuwa yakitoa heshima kwa balozi wa Marekani alieuawa mjini Benghazi wiki iliyopita, Christopher Stevens, yakiwa na maneno kama vile, " Libya ilimpoteza rafiki," na "Tunataka haki kwa Stevens."

Waandaji waliitishwa maandamano hayo kuitaka serikali kuu mjini Tripoli ichukua hatua za kuyadhibiti makundi ya yenye silaha ambayo yameendelea kuwa na ushawishi mkubwa hata baada ya kumalizika uasi uliyomuondoa madarakani na kisha kumuua aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Ghadafi. Maandamano pinzani ya Ansar al-Sharia yalivuta mamia waliyokuwa wakipunga bendera nyeusi na nyeupe zilizoandikwa na kalima ya tamko la imani kwa waumini wa kiislamu.

Balozi Christopher Stevens aliyepoteza maisha pamoja na maafisa wengine watatu wa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi Septemba 11 mwaka huu.
Balozi Christopher Stevens aliyepoteza maisha pamoja na maafisa wengine watatu wa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi Septemba 11 mwaka huu.Picha: AP

Ansar al-Sharia na vurugu za Septemba 11

Ansar al-Sharia inatuhumiwa kushiriki uvamizi wa Septemba 11 dhidi ya ofisi ya uwakilishi ya Marekani mjini Benghazi ambapo balozi Chris Stevens na maafisa wengine watatu walipoteza maisha. Lakini kundi linakanusha kuhusikana vurugu hizo. Siku ya Ijumaa,kwa mara ya kwanza waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani,Hillary Clinton, alilitaja tukio hilokuwa ni la kigaidi.

"Hakuna mungu isipokuwa Allah," walikuwa wakisema waandamanaji hao na pia, "Obama ni adui wa Mwenyezi Mungu." Ufaransa na Marekani zinatushambulia kwa kumdhihaki mtume wetu na vinginevyo, alisema Mohammed Abdullah, mwenye umri wa miaka 30. Kundi la Ansar al-Sharia ambalo lilikataa kujiunga na vikosi vya usalamavya taifa, lilikuwa linapinga filamu ya Innosence of Muslims iliyotenegenezwa na wamarekani wa madhehebu ya koptik na vikaragosi vinavyomuonyesha mtume Muhammad.

Mwandishi:Iddi Ismail Ssessanga/afpe

Mhariri: Sekione Kitojo