1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Klabu za waandishi Tanzania zalaani polisi kuwapiga

Sylvia Mwehozi
15 Agosti 2018

Umoja wa klabu ya waandishi wa habari  nchini humo (UTPC ) umelaani hatua ya jeshi la polisi kuwakamata na kuwapiga waandishi wa habari wakiwa katika hatua ya kutekeleza majukumu yao ya kazi.

https://p.dw.com/p/33BiA
Tansania Polizei auf Straße
Picha: DW/Ericky Boniphace

Nchini Tanzania, wiki za hivi karibuni kumeshuhudiwa waandishi wa habari wawili nchini humo katika mikoa ya Mara na Dar es Salaam wakijikuta katika kadhia ya jeshi la polisi wakati wakitimiza majukumu yao ya uandishi. 

Mkurugenzi mtendaji wa UTPC Karsin Abubakari ameeleza hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza mara baada ya waandishi wawili Sitta Tuma wa gazeti la Tanzania daima na Silas Mbise wa wapo radio kukamatwa na kupigwa na jeshi la polisi wakati wakitekeleza majukumu yao ya kazi

Ameongeza kwa kusema kuwa mara baada ya matukio ya kukamatwa kwa waandishi wa habari Tanzania, chama hicho kiliamua kuliandikia barua  jeshi la polisi ikiwemo mkuu wa jeshi hilo Inspekta Jenerali Simon Sirro lakini hawajawai kujibiwa jambo linalozua sintofahamu kwa wandishi wa habari nchini humo.

Tansania Polizei attackiert einen Journalisten in Dar es Salaam
Polisi wakiwa wamemdhibiti mwandishi wa habari Picha: Article19-East Africa

Kwa upande wake  Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania daima, Sitta Tuma ambaye agosti 8 alishikiliwa na jeshi la polisi mkoani mara na kufunguliwa mashita kwa madai kuwa amefanya mkusanyiko usiokuwa na uhalali wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi amesema  wakati umefika kwa jeshi la polisi kujitathimini na kufuata sheria na taratibu za nchi .

Katika hatua nyingine Sitta amemuomba mkuu wa jeshi la polisi nchini humo na Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola wajitafakari na kuangalia namna za kulibadilisha jeshi hilo hili kuleta mabadiliko ya kiutendaji kwa askari wa jeshi la polisi nchini Tanzania

Matukio ya kukamatwa na kupigwa kwa waandishi wa habari nchini Tanzania yanaelezwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari na wana habari nchini humo ambapo inadaiwa kuwa baadhi ya waandishi wa habari wanahofia kutekeleza majukumu yao katika taifa hilo la afrika mashariki.

Mapema mwezi huu matukio mawili yalilipotiwa nchini tanzania ambapo wandishi wawili wa habari walishikiliwa na kushambulia na jeshi la polisi wakati wakitekeleza majukumu yao jambo ambalo limewaibua umoja wa club za wandishi wa habari nchini Tanzania ambao wamelaani matukio hayo nakulitaka jeshi la polisi kufanya mabadiliko ya haraka.

Mwandishi: Dotto Bulendu

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman