1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi waendelea kumiminika kushuhudia uchaguzi Zimbabwe

Sekione Kitojo
26 Juni 2018

Licha ya shambulizi la bomu mwishoni mwa wiki, serikali ya Zimbabwe imeapa kuendelea na uchaguzi wake wa kwanza tangu nchi hiyo kupata uhuru bila ya kiongozi wake wa muda mrefu Robert Mugabe.

https://p.dw.com/p/30Job
Simbabwe Bombenanschlag
Picha: Getty Images/AFP/Z. Auntony

Msemaji wa polisi, Charity Charamba, alisema jana kwamba mripuko huo ambamo Rais Emmerson Mnangagwa alinusurika katika mkutano wa hadhara mwishoni mwa wiki mjini Bulawayo ulisababisha watu wawili kuuwawa. 

Waangalizi kutoka nchi 46 na mashirika 15 ya kikanda na kimataifa wanatarajiwa kuangalia uchaguzi huo wa rais na bunge uliopangwa kufanyika Julai 30. 

Uchaguzi wa rais unawakutanisha Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75 wa chama tawala cha ZANU-PF dhidi ya chama cha muda mrefu cha upinzani cha MDC ambacho mgombea wake ni Nelson Chamisa mwenye umri wa miaka 40.

Uchunguzi wa maoni unaonesha uwezekano wa kuwepo na ushindani mkubwa.