1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi 150 wa Kikurd wauwawa.

26 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CgI1

Istanbul. Jeshi la Uturuki limedai kuwa limeshambulia zaidi ya maeneo 200 ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq katika muda wa siku 10 zilizopita na kuuwa mamia kadha ya waasi. Jeshi hilo limesema katika taarifa iliyotolewa katika wavuti ya jeshi kuwa zaidi ya waasi 150 wameuwawa katika mashambulizi ya anga Desemba 16 pekee.

Afisa kutoka jeshi la ulinzi la Wakurd wa Iraq amesema kuwa ndege za kivita za Iraq zimefanya mashambulizi kaskazini mwa Iraq Jumanne lakini amedai kuwa vijiji vilivyolengwa vilikuwa havina watu.

Tangu mwaka 1984, uasi wa kijeshi wa kundi la PKK dhidi ya Uturuki wakitaka kujitenga kwa jimbo hilo la Wakurd umesababisha zaidi ya vifo 37,000. Kundi hilo linatambulika kama kundi la kigaidi na Uturuki , Marekani na umoja wa Ulaya.