1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa FNL wasimamisha mpango wa kuwakusanya wanajeshi wake

7 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EXR0

BUJUMBURA

Waasi wa kundi la FNL Palipehutu nchini Burundi wamefutilia mbali mpango wa kuwakusanya wapiganaji wake wakipinga hatua ya serikali ya kukataa kulitambua kundi hilo kama chama cha kisiasa.Kiongozi wa kundi hilo Agathon Rwasa ametoa tangazo hilo hapo jana akisema hawawezi kuendelea na mpango huo wakati serikali haifanyi lolote na inaendelea kuliangalia kundi hilo kama la waasi kuliko la kisiasa. Kundi la FNL lilianzisha mpango wa kuwakusanya wanajeshi wake mwezi juni 16 na kuwapeleka kiasi wapiganaji wake 150 kaskazini magharibi mwa Burundi.Kwa mujibu wa makubaliano ya amani ya hivi karibuni yaliyosimamiwa na Umoja wa Ulaya na Uswisi kundi la FNL lilitakiwa kuwakusanya wanajeshi wake katika eneo la magharibi na kaskazinimagharibi mwa nchi.