1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi waalikwa mkutamo wa amani Congo

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdw9

KINSHASA

Viongozi wa makundi mbali mbali ya waasi na wanamgambo wanaoendesha harakati zao katika Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo wamealikwa katika mkutano wa amani kaskazini mwa nchi hiyo.

Spika wa bunge la taifa Vital Kamerhe ameiambia radio ya Umoja wa Mataifa Okapi kwamba mkutano huo wa siku tisa utakaoanza hapo tarehe 27 mwezi wa Desemba katika mji mkuu wa Kivu Kaskazini wa Goma utawakutanisha wale wenye kupendelea hoja ya amani na wale wenye kuunga mkono hoja ya vita.

Miongoni mwa walioalikwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Generali wa zamani Laurent Nkunda kiongozi wa waasi ambaye vikosi vyake vilijipatia ushindi mkubwa katika mapambano ya hivi karibuni dhidi ya vikosi vya serikali.