1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wadai kudhibiti mji wote wa Tripoli

28 Agosti 2011

Vikosi vya waasi nchini Libya vinadai vimeweza kuudhibiti mji wote wa Tripoli baada ya siku sita tangu kuingia mjini humo, wakiendelea kumsaka kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi.

https://p.dw.com/p/12OrH
Waasi katika viunga vya TripoliPicha: dapd

Msemaji wa waasi alisema kikosi cha mwisho cha Gaddafi kimetimuliwa katika mji huo na kwamba maisha yameanza kurejea katika hali ya kawaida licha ya taariza za ukosefu wa umeme, maji, na chakula. Hali hiyo imekuja wakati jitahada za kumsaka Gaddafi zikiendelea, huku bado haijulikani wapi kiongozi huyo alipo.

Hapo jana zilipatikana taarifa kwamba mlolongo wa magari sita yenye silaha ulivuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Algeria. Hata hivyo bado haijafahamika iwapo Gaddafi na watoto wake ama maafisa wengine wa serikali ya Libya walikuwemo katika gari hizo.

Mwandishi:Sudi Mnette