1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wadhibiti upya miji muhimu Libya

27 Machi 2011

Majeshi ya muungano wa kimataifa yameshambulia vikosi vya nchi kavu vya Libya na vituo vingine katika eneo la mwambao wa Bahari ya Mediterania.

https://p.dw.com/p/RD1Y
In this image provided by the French Defense Ministry, French soldiers check a Mirage 2000 jet fighter before a mission to Libya, at Solenzara air base, Corsica island, Mediterranean Sea, Monday March, 21, 2011. The air campaign by U.S. and European militaries has unquestionably rearranged the map in Libya and rescued rebels from the immediate threat they faced only days ago of being crushed under a powerful advance by Gadhafi's forces. (Foto:Anthony Jeuland; Sirpa Air/AP/dapd) NO SALES
Wanajeshi wa Ufaransa wakijiandaa kwa operesheni ya LibyaPicha: AP

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Marekani mjini Washington, vikosi hivyo vya muungano wa kimataifa, vile vile vimehujumu miji ya Tripoli, Misrata na Ajdabiya.

Waasi wa Libya wakisaidiwa kutoka angani na ndege za muungano huo wa kimataifa, wamefanikiwa kuudhibiti tena mji muhimu wa Ajdabiya.

Ushindi wa wapinzani hao wa serikali ya kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi, unatazamwa kama ni ishara kuwa mapambano ya kuidhibiti nchi hiyo, yanachukua mkondo mpya. Vikosi shirika vya Ufaransa vimesema kuwa vimeteketeza ndege saba na helikopta mbili zilizokuwepo kwenye kituo cha jeshi la anga huko Misrata.