Waasi waunda chama kipya mashariki mwa Kongo
8 Mei 2012Matangazo
Chama hicho kimeundwa na viongozi wa ngazi ya juu wa zamani wa waasi wa Chama cha CNDP na kinaongozwa na Kanali Makenga Sultani, naibu kamanda wa zamani wa CNDP kabla ya wapiganaji wa chama hicho kujiunga na jeshi la DRC hapo Januari 2009. Kuundwa kwa chama hicho kunadhaniwa kuwa huenda kutasababisha vurugu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuendelea.
John Kanyunyu, mwandishi wetu katika eneo hilo, ametutumia ripoti ifuatayo kutoka Goma
(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: John Kanyunyu
Mhariri: Othman Miraji