1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge wa Uingereza waanza mjadala kuhusu mpango wa Brexit

9 Januari 2019

Wabunge wa Uingereza leo wanaanza mjadala wa siku tano kuhusu mpango wa Waziri Mkuu Theresa May wa kuondoka katika Umoja wa Ulaya, Brexit, mpango ambao unakabiliwa na upinzani mkubwa.

https://p.dw.com/p/3BEgl
May verschiebt Brexit-Abstimmung
Picha: picture alliance/empics

Serikali ya Uingereza leo imeshindwa bungeni katika mchakato wa kura ya mabadiliko ya kiutaratibu ambayo yanapunguza muda wa  kurejea na mpango mbadala iwapo ule wa Waziri Mkuu Theresa May,wa Brexit utashindwa kupitishwa wiki ijayo. Hatua hiyo inajaribu kuilazimisha serikali hiyo kurejea bungeni baada ya siku tatu na mpango mbadala badala ya siku 21 zilizotajwa katika sheria ya Brexit.

May leo amesema anashinikiza mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Ulaya kupata hakikisho ili kupunguza wasiwasi kufuatia mpango wake wa Brexit. Vile vile amesema serikali yake inatafuta njia za kulipa bunge nguvu zaidi kufuatia mazungumzo ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kuhusu uhusiano wa baadaye, ikiwemo kuongeza kipindi cha mpito badala ya kuchochea sera ya kusimamia sheria ya masuala ya forodha kati ya Ireland ya Kaskazini na Jamhuri ya Ireland.

London Unterhaus berät über Brexit
Picha: picture-alliance/empics

May amesema kwamba, " Tumekuwa tukitathmini jinsi bunge linaweza kupewa jukumu kubwa wakati tukiendeleza mashauriano ya hatua inayifuatia, hivyo naweza kuliambia bunge kwamba iwao uhusiano wetu wa baadaye au makubaliano mbadala hayatakuwa tayari ifikapo mwaka 2020, linawzea kupiga kura kuhusu iwapo litataka kuongeza muda wa utekelezwaji. Nina furaha kurejelea nilichokisema awalikwamba tutaondoka katika Umoja wa Ulaya tarehe 29 Machi. Nataka tuondoke na mpango mzuri ambao nimeuwasilisha."

Serikali ya Uingereza ilitangaza jana kwamba wabunge hao watapiga kura Jumanne wiki ijayo tarehe 15 kuhusu makubaliano ambayo May aliyafikia na Umoja wa Ulaya , huku ikikanusha madai kuwa huenda ikataka mpango huo ucheleweshwe iwapo makubaliano yatakataliwa.

May verschiebt Brexit-Abstimmung
Picha: picture alliance/empics

Inadaiwa kwamba kwa wiki kadhaa Uingereza imekuwa ikijadili uwezekano huo, lakini Waziri wa Brexit Stephen Barclay amekanusha ripoti hizo akisema kuna baadhi ya watu katika Umoja wa Ulaya wanaojadili suala hilo lakini huo sio msimamo wa serikali ya Uingereza. Wakati huo huo Waziri wa Ufaransa katika umoja huo Nathalie Loiseau amesema hakuna zaidi wanachoweza kukifanya na kuonya dhidi ya kuwa na imani kubwa katika mazungumzo kuhusu kupanua kifungu cha hamsini cha mpango huo. 

Wanaounga mkono mpango wa Brexit wana wasiwasi kwamba hakuna mbinu ya Uingereza kujiondoa peke yake, ikimaanisha kwamba huenda ikasalia katika umoja huo milele hivyo kuathiri uwezo wake wa kuafikia makubaliano na mataifa mengine duniani. 

Mwandishi: Sophia Chinyezi/AFPE

Mhariri: Saumu Yusuf