1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachezaji wa Ujerumani walitumia dawa za kuongeza nguvu

5 Agosti 2013

Ripoti ya uchunguzi kwamba iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi iliendesha mipango ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni katika miaka ya 1970, ikiungwa mkono na serikali, imechapishwa

https://p.dw.com/p/19KAf
ARCHIV - ILLIUSTRATION - Das Symbolfoto zeigt eine Spritze vor dem Wort Doping, aufgenommen am 25.07.2007. Die grün-rote baden-württembergische Landesregierung will den Druck auf Dopingsünder erhöhen. Dazu stellt Justizminister Stickelberger (SPD) am 13.11.2012 entsprechende Eckpunkte vor, die die strafrechtliche Bekämpfung von Doping verbessern sollen. Im Kampf gegen unerlaubte leistungssteigernde Mittel ist Baden-Württemberg nach Bayern das zweite Bundesland, das eine Schwerpunktstaatsanwaltschaft zur Verfolgung von Dopingdelikten eingerichtet hat. Foto: Patrick Seeger/dpa (Zu lsw Vorausmeldung: «Land will Druck auf Dopingsünder erhöhen» vom 13.11.2012) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Doping SymbolbildPicha: picture-alliance/dpa

Mradi uliofadhiliwa na serikali wa dawa za kuongeza nguvu mwilini pia ulitumiwa katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki, lakini ripoti ya utafiti uliofanywa na jopo kutoka chuo kimoja kikuu mjini Berlin pia imesema kiwango cha matumizi ya dawa hizo kilikuwa cha kutisha katika iliyokuwa Ujerumani ya Mashariki.

Kwa kuzingatia mahojiano yaliyofanywa na zaidi ya mashahidi 50, timu kutoka chuo kikuu cha Humboldt kilitumia miaka mitatu kufanya utafiti wa ripoti yenye kurasa 800 uliopewa kichwa “matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini nchini Ujerumani kuanzia mwaka wa 1950 hadi leo”.

Ripoti hiyo inadai kuwa baadhi ya wanasiasaw wakati huo walijua kuhusu mpango huo na kuna shahidi mmoja aliyesema kuwa waziri mmoja wa mambo ya ndani ambaye hajatajwa jina lake alisema kuwa “wanariadha wao wa iliyokuwa Ujerumani ya magharibi walistahili kuwa na mazingira sawa ya kabla ya ushindani na wenzao wa mashariki.”

Huyu hapa waziri wa zamani wa mambo ya ndani Gerhard Groß anasema "Kile ambacho kimesababisha nchi nyingine kupata mafanikio katika mazoezi na mashindano ya kimataifa, kimewanyima wachezaji wetu fursa".

Ripoti hiyo haijachapishwa, lakini sehemu ya utafiti huo kuanzia mwaka wa 2012, imechapishwa na gazeti moja la Ujerumani suddeutsche zeitung ambalo lilifichua Jumamosi kuwa matumizi ya dawa hizo yalifanywa katika vitengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na riadha na kabumbu.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Christoph Bergner anasema matokeo ya mwisho yanastahili kupitiwa kabla ya kuchapishwa. Anasema "wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani haijapinga kufanya uchunguzi kuhusu suala hilo. Tumekuwa tukiunga mkono taasisi ya michezo na sayansi kwamba mahitaji ya kuzuia utoaji wa data lazima ulindwe.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman