1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wachunguzi wa Scotland Yard wawasili Pakistan.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkQ6

Islamabad.

Wachunguzi wa kitengo cha kupambana dhidi ya ugaidi kutoka katika jeshi la polisi la Uingereza kinachojulikana kama Scotland Yard wamewasili nchini Pakistan kusaidia kuchunguza mauaji ya kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto. Rais wa Pakistan Pervez Musharaf amekana madai kuwa serikali yake inahusika na kuuwawa kwa kiongozi huyo, akisema kuwa hakuna kinachofichwa na kwamba Bhutto ameonywa mara kadha juu ya vitisho kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu. Kuuwawa kwa Bhutto wiki iliyopita kumezusha wasi wasi wa usalama miongoni mwa vyama vya upinzani ambao wanadai kupatiwa ulinzi zaidi kabla ya uchaguzi mkuu ambao umeahirishwa hadi February 18.