1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

wafanyakazi wa kujitolea ambao wamehukumiwa nchini Chad kwa kuwateka nyara watoto warejea nyumbani

28 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/ChYB

NDJAMENA:

Wafanya kazi za misaada sita ambao walihukumiwa miaka minane kila mmoja nchini Chad, kwa kuwateka nyara watoto 103 wameondoka kwa ndege kuelekea nyumbani kwao Ufaransa kutumikia kifungo chao huko.

Serikali ya Ufaransa iliiomba Chad kuwarejesha nyumbani wanaume wanne na wanawake wawili.

Walikuwa wanatumikia shirika lisilolaserikali la Zoe’s Ark.Watu hao watarejeshwa Ufaransa kulingana na mkataba wa kisheria wa nchi hizo mbili wa mwaka 1976.

Wafanya kazi hao walidai kuwa walikuwa wanasaidia kuwaokoa watoto hao mayatima,hata hivyo watoto karibu wote walikuwa wametoka katika familia ambazo baado ni hai na kuwa walishawishiwa kutoa watoto hao kwa ajili ya kupelekwa Ufaransa.