1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa Kishia waadhimisha Ashura

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cuzo

BAGHDAD: Nchini Irak,kiasi ya mahujaji milioni 2 wameandamana katika mji wa Karbala kuadhimisha Ashura,siku mojawapo takatifu kwa wafuasi wa madhehebu ya Kishia.Usalama umeimarishwa katika mji wa Karbala,wakiwepo zaidi ya wanajeshi na askaripolisi 20,000 ili kuzuia machafuko.Hali ya mvutano imezuka baada ya watu darzeni kadhaa kuuawa katika mapambano ya siku ya Ijumaa kati ya polisi na wafuasi wa madhehebu ya Kishia katika miji ya Basra na Nasiriyah,kusini mwa Irak.Mwaka uliopita,watu 263 waliuawa katika mapambano yaliyozuka kati ya polisi na wafuasi wa madhehebu ya Kishia.Ashura huadhimishwa kwa siku 10, kuomboleza kifo cha Imam Hussein.