1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafugaji wageukia kilimo nchini Kenya

17 Juni 2015

Athari za mabadiliko ya tabia nchi ulimwenguni sio tu kuwa zinaikausha misitu iliyokuwa imezagaa maeneo mbalimbali duniani.

https://p.dw.com/p/1Fik8
Massai in Kenia QUALITÄT
Picha: DW/A.Wasike

Bali pia inakausha na kugeuza mila na tamaduni za jamii za wanaadamu na kuwafanya sasa kugeukia mifumo mipya ya maisha ambayo hawaikuwahi kuwepo hapo awali.

Katika tamasha la utamaduni la Marsabit na Ziwa Turkana lilioandaliwa katika kaunti ya Marsabit nchini Kenya, Mariam Lemuska hakusikiliza ngoma au muziki. Badala yake,alijifunza kupika injera, ambacho ni chakula maarufu cha Waethiopia.

Lemuska mwenye umri wa 39 anatokea jamii ya wafugaji ambayo wanaishi kwa kutegemea zaidi nyama, maziwa na damu ya mnyama. Lakini jambo baya zaidi ni ukame ambao unasababisha vifo vya wanyama, na sasa Lemuska yuko tayari kutafuta njia mpya ya kuweza kulisha familia yake.

"Wanyama wetu kila siku wanakufa wakati ukame unapokuwa mkubwa, na kutuacha sisi na njaa. Nahitaji kujifunza njia mbadala ya kuweza kuishi," alisema mwanamke huyo.

trockenes Maisfeld
Picha: CC BY-NC-SA 2.0/C. Schubert (CCAFS)

Kwenye maonyesho haya ya utamaduni, Lemuska aliangalia vyema wakati afisa wa kilimo akionyesha baadhi ya vyakula kama vile mtama, keki ya maziwa na asali na chapati zinazotengenezwa kwa maboga.

Mara moja kwa mwaka, jamii kubwa ya Kaunti ya Marsabit, Kaunti kubwa nchini Kenya hukusanyika na kusherehekea urithi wao. Lakini kutokana na mabadiliko ya tabia nchi kutokea katika maeneo kame kama kulivyo Turkana, mkusanyiko huu pia umegeukia na kuwa maonyesho ya mbinu zinazoweza kutumiwa ili kukabiliana na mazingira yanayobadilika katika kanda hiyo.

"Ni lazima tutumie fursa ya idadi ya watu waliopo hapa, kwa sababu ni changamoto kufikia kila mtu kutokana na ukubwa wa kaunti, miundombinu duni na uduni wa mawasiliano na simu." alisema Guyo Galicha Iyya mratibu wa masula ya ukame wa Kaunti.

Katika maonyesho, maafisa kutoka kaunti za serikali kuwashauri watu kufuga wanyama kama mbuzi na hasa aina ya kondoo badala ya ng'ombe, kwa sababu wanyama wadogo wanakula na kunywa kidogo na kuimili ukame.

Katika hatua nyingine watu kufundishwa jinsi ya kuvuna maji ya mvua,na jinsi ya kupanda mazao yanayovumilia ukame ikiwa ni pamoja na kuonyesha baadhi ya maeneo yaliyoendelea na Shirika la utafiti wa kilimo na mifugo la nchini Kenya, ikiwa ni njia mbadala kwa ufugaji.

Kampf gegen Bodenerosion in Kenia
Picha: Das Fotoarchiv

Siku tatu za tamasha, ambalo hufanyika katika kitongoji cha Loiyangalani, ulianzishwa na utawala wa ndani mwaka 2008 kama njia ya kukuza amani miongoni mwa jamii za wafugaji katika kaunti, na kusherehekea urithi wao wa kitamaduni.

Jamii za makabila ambayo mara kwa mara yanahudhuria ni pamoja na El Molo, Warendille, Samburu, Turkana, Dassanatch, Gabra, Borana, Konso,Sakuye, garee, Waata, Burji na watu wa Somalia.

Tamasha linalenga katika muziki na utamaduni. lakini kuongezeka Umati kutokana na maonyesho juu ya mabadiliko ya tabia nchi ni wazi inaonyesha dalili ya kuongezeka kwa wasiwasi kwa watu wa Kaunti na Viongozi.

Marsabit ina idadi ya watu 300,000 ambao wameenea katika eneo la kilomita za mraba71,000 . ikilinganishwa na Kaunti ya Mombasa , yenye watu milioni moja na kilimita za mraba 219.

Kila siku tulikuwa tunayategemea mashirika yasiyo ya kiserikali
na wanaojitolea kuwafikia watu wanaoishi mbali na kila mmoja, "alisema Samana

Kupata taarifa kwa familia ni vigumu hasa kwa sababu karibu wakazi wote wa Marsabit ni wafugaji na wanaishi maisha ya kifugaji, alisema.

Aliongeza kuwa kila siku wanahama hama kwa ajili ya kutafuta malisho, na kufanya kuwa vigumu kuwaleta pamoja kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa aina wowote .

Aidha Mratibu wa masuala ya Ukame Iyya alisema kuwa, Umbali mrefu pia kunafanya iwe vigumu kwa wakazi kufika mjini kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.

Mwandishi: Salma Mkalibala/RTRE

Mhariri: Mohammed Khelef