1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki kwa waliopotea wakati wa Jammeh Gambia

28 Februari 2017

Baada ya kumalizika kwa utawala wa zaidi ya miongogo miwili wa rais Yahya Jammeh, Wagambia sasa wameanza kutafuta haki kwa ndugu na jamaa waliotoweka wakati wa utawala huo wa kikandamizi uliofikia tamati mwezi Januari.

https://p.dw.com/p/2YOQx
Gambia Präsident Adama Barrow | Amtsübernahme & Einweihungszeremonie in Bakau
Raisi wa Gambia Adama BarrowPicha: Reuters/T. Gouegnon

Polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi katika visa kadhaa, lakini wadadisi wanasema kufungua mashtaka katika mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC ni changamoto kubwa.

Wakati afisa wa usalama wa Gambia alipomkamata mwandishi wa habari Ebrima Manneh ofisini kwakwe, alimwambia mlinzi wa ofisi amuwekee chai yake.  "Narudi sasa hivi," alisema Ebrima kulingana na mfanyakazi mwenziwe Alhagie Jobe ambaye alikuwepo katika chumba cha habari. Siku hiyo  ilikuwa ni mchana wa Julai 11, 2006; na tangu wakati huo Ebrima hakuonekana tena na familia yake na hata wafanyakazi wenzake katika gazeti la Daily Observer. Mashirika ya haki za binaadamu yanasema  Manneh ni moja kati ya wagambia  ambao waliotoweshwa wakati wa utawala wa miaka 22 wa rais Yahya Jammeh ambao ulimalizika mwezi Januari alipoikimbia Gambia.

Jamaa wa Manneh wamejaribu sana kumtafuta mwandishi huyu ambaye kwa jina la utani anajulikana kama "chief," ingawa hakuwa na wadhifa wowote wa kikabila. Na sasa jamaa  hao wanaami kuwa ameuwawa na kama ilivyo kwa wagambia wengi, wao pia wanataka haki itendeke.

"Nataka serikali mpya ichukue hatua na iwahukumu watu wote waliohusika na upoteaji wa ndugu yangu," alisema Adama Manneh ambaye ni dada wa mwandishi huyo, ambaye pia  ni afisa wa polisi huku akiwa amevaa fulana yenye picha ya ndugu yake na maandishi yasemayo: "Yuko wapi Chief Manneh?" Ndugu wa kiume wa Ebrima, Lamin, alisema anatumaini angalau kuupata mwili wake.

Baadhi ya familia zinatarajia kukusanya ushahidi kwa ajili ya kumfungulia mashitaka rais huyo wa zamani Yahya Jammeh -ambaye aliachia madaraka kufuatia shinikizo kubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwezi Desemba - kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ikiwemo kufungwa watu kinyume cha sheria, mateso na mauaji ya wapinzani wake, madai ambayo hata hivyo yanapingwa na wafuasi wake.

Ex-Präsident Jammeh verlässt Gambia
Yahya Jammeh akiondoka GambiaPicha: Picture-Alliance/dpa/J. Delay

Maafisa wa haki wamesema hata hivyo kufungua mashitaka dhidi ya Jammeh inaweza kuwa vigumu. Kiongozi mwengine wa zamani wa Kiafrika, rais wa zamani wa Chad Hissene Habre alifungwa kifungo cha maisha mwaka jana kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, zaidi ya robo karne baada ya kuondolewa madarakani. Habre alitiwa hatiani na mahakama nchini Senegal kwa msaada wa nyaraka zilizomtia hatiani, lakini maafisa wa haki za binadamu mpaka sasa hakuna ushahidi madhubuti uliopatikana dhidi ya Jammeh.

Watu wengi nchi Gambia wanataka Jammeh afikishwe mahakama ya kimataifa ICC. Lakini Guinea ya Ikweta si mwanachama wa ICC na hakuna matarajio kama watamtoa Jammeh.  Polisi imeahidi kuzifanyia upelezi kesi 30 za watu walioripotiwa kupotea tangu 1994 wakati Jammen alipochukua madaraka.  Rais wa Gambia Adama Barrow ameahidi kushughulikia mashitaka hayo ya zamani ikiwemo mashitaka ya mateso, akisaidiwa na umoja wa mataifa. Rais huyo pia ameanza kufanya mageuzi katika taasis muhimu za taifa ikiwemo hatua yake ya karibuni kumuondoa mkuu wa zamani wa majeshi Jenerali Ousman Badjie pamoja  na maafisa kadhaa wa ngazi ya juu jeshini, ambao walikuwa nguzo muhimu katika utawala wa Jammeh.

Familia ya Manneh mapaka sasa hawaijui sababu za kukamatwa kwake, lakini wafanya kazi wenziwe wanafikiria ni kutokana na habari alizokuwa akiziandiaka juu ya raisi huyo wa zamani. Mahakama ya kanda ya  ilioko nchini Nigeria, ilisikia kuwa kuwa Manneh alihamishwa  magezera mara sita kati ya 2006 na 2008. Na hakuwahi kufikishwa mahakamani hata mara moja.

Kila mwaka Adama alikwenda gereza kuu la Banjul kuhudhuria kuachiwa kwa wale waliopewa msamaha na kuachiwa huru, kuona kama ndugu yake atakuwa miongoni mwao. Matumaini yake yalikatika kabisaa wakati raisi mpya alipowaachia huru wafungwa wa kisiasa  100 na Manneh hakuwa miongoni mwao.

"Nilidhani kuwa ndugu yangu pia ataachiwa huru, lakini hakuwemo katika watu hao,najua ameuliwa." alisema Adama huku akitokwa na machozi

Mwandishi: Najma Said

Muhariri: Iddi Ssessanga