1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wageni kuchukuliwa alama za vidole vyote 10

11 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZyX

Wageni wanaokwenda Marekani,watapaswa kuchukuliwa alama za vidole vyote kumi kwa mashine ya elektronik.Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani,Michael Chertoff ameanzisha utaratibu huo wa usalama katika uwanja wa ndege wa Washington Dulles.Amesema,hadi mwisho wa mwaka 2008,viwanja vyote vya ndege vya kuingilia Marekani vitakuwa na mtambo huo.

Alama za vidole kumi zinazochukuliwa zitahifadhiwa kwa muda wa miaka 75.Hivi sasa wageni wanaoingia Marekani huchukuliwa alama za vidole vya pili vya kila mkono tu.