1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini Kenya wagoma

John Juma
2 Novemba 2017

Wahadhiri wanagoma wakipinga kile wanachokiita kushindwa kwa serikali  kutekeleza makubaliano ya mwezi Machi kuongeza mishahara yao na mafao ya nyumba.

https://p.dw.com/p/2muBN
Die Universität in Nairobi
Picha: CC BY-SA 3.0 Wing

Wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini Kenya wameanza mgomo wakipinga kile wanachokiita kushindwa kwa serikali  kutekeleza makubaliano ya mwezi Machi kuongeza mishahara yao na mafao ya nyumba.

Mgomo huo ulioanza jana unaweka mbinyo zaidi dhidi ya serikali baada ya mgomo wa wauguzi katika hospitali za umma katika  muda wa miezi michache iliyopita ambayo imedhoofisha kazi za huduma ya afya katika nchi hiyo.

Hali hiyo pia inadhoofisha zaidi hali ya baadaye zaidi ya wanafunzi nusu milioni katika vyuo vikuu 31 vya umma nchini Kenya, tangu  pale wahadhiri walipomaliza mgomo wao wa siku 54 kuhusiana na nyongeza ya mishahara mwezi Februari na kutia saini  makubaliano na serikali mwezi Machi.

Wafanyakazi wote wanaohusika na masomo katika vyuo vikuu 31 vya umma wamo katika mgomo kuanzia jana tarehe mosi  Novemba, Constantine Wasonga, katibu mkuu wa umoja wa wafanyakazi wa vyuo vikuu, amesema katika taarifa iliyopatikana na  shirika la habari la Reuters leo. Maafisa wa serikali hawakupatikana mara moja kutoa maelezo.