1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 64 wa Kiafrika wazama nchini Yemen

23 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS9Y

Wahamiaji 64 wa Kiafrika wamezama katika Ghuba ya Aden wakati wakijaribu kuvuka kutoka Somalia kuingia Yemen.

Miili yao imeopolewa kutoka baharini na wavuvi pamoja na walinzi wa mwambao wa Yemen baada ya mashua ya wahamiaji hao kupinduka nje ya pwani ya jimbo la Chabwa kusini mashariki mwa nchi hiyo.Shirika la habari la serikali nchini Yemen la Saba limesema wahamiaji 25 wasio halali waliweza kukoga hadi ufukweni.

Bado hakuna taarifa juu ya uraia wao lakini kila mwaka mamia ya Waethiopia na Wasomali wanakufa wakati wakijaribu kuvuka katika safari hiyo ya hatari.